January 09, 2014
NOAH YAUA WAWILI MKATA NA KUJERUHI NANE 
Na Oscar Assenga, Handeni.
WATU wawili wamefariki dunia hapo hapo na wengine nane kujeruhiwa
baada ya gari aina ya  Noah walilokuwa wamepanda kutaka kulipita gari
lililkuwa mbele yake na kukutana na gari lori aina ya Volvo na
kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo hivyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Costastine Massawe  athibitisha
kutokea tukio hilo leo na kueleza tukio hilo lilitokea majira ya saa
tano mchana wakati gari hilo aina ya Noah T266 AXZ lililokuwa
likitokea Kabuku kwenda Mkata ambapo lilipofika eneo la kwamgogo ndio
lilipotaka kulipita gari lililokuwa mbele yake na ndipo alipkutana na
lori aina ya  Volvo na kugongana nalo.

Massawe amtaja dereva wa gari aina ya Noah aliyesababisha ajali hiyo
kuwa ni Abdallah Selehe (60) mkazi wa kata ya Hale wilayani Korogwe
mkoani Tanga ambaye alikimbizwa kwenye hospitali ya Mkata Handeni
akiwa hajitambui akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.

Aliwataja watu waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni wanawake
wawili ambao walikuwa miongoni mwa abiria waliokuwepo kwenye gari hilo
aina ya Noah ambapo kwa mujibu wa kamanda masawe majina yao haya
kuweza kupatikana mara moja.

Kamanda Massawe alisema chanzo cha ajili hiyo ni dereva za gari hilo
aina ya Noah kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake kwenye kona na
ndio ambapo alipokutana uso kwa uso na lori hilo na kusababisha ajali
hiyo.

    "Ajali nyingi zinatokea kutokana na madereva kutokuwa makini kwani
wengi wao wanasababisha ajali hizo kwa kutaka kuyapita magari yaliyopo
mbele yao bila kufikiria kufanya hivyo ni kukiuka sheria za usalama
barabarani "Alisema Kamanda Massawe.

Aidha kamanda  Massawe alitoa wito madereva mkoani Tanga kutii sheria
bila kuruti kwa kufuata sheria za usalama barabarai na kuwataka abiria
kuacha kushabikia mwendokasi badala yake watoe taarifa kwa jeshi hilo
ili hatua kali ziweze kuchukuliwa zidi yao

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »