NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
WASANII Nguli wa Filamu hapa nchini wametakiwa kuacha kuwabagua wasanii wachanga badala yake washirikiane nao ili kufanya nao kazi kwa pamoja lengo likiwa ni kusukuma gurudumu la maendeleo yao.
Ushauri huo ulitolewa leo na Msanii kipukizi wa
Filamu mkoani Tanga,Mohamed Kilua “Action Made”ambaye hivi sasa anatamba katika
tasnia hiyo hapa nchini.
Kilua ambaye anatamba katika filamu za Kata K
aliyocheza na Mzee King Majuto,Gentlemen aliyoshirikiana na Richie Mtambalike
na Impossible aliyecheza na marehemu Sharomilionea pamoja na kitale.
Alisema katika filamu hiyo ya kata K alicheza yeye
kama ndio muongozaji wakati nyengine alishiriki kwenye upande tofauti tofauti .
Kilua alisema changamoto kubwa inayowakabili wasanii
wachanga ni ulipwaji umekuwa sio mzuri kutokana na kulipwa malipo kidogo ambayo
hayalingani na kazi wanayoifanya.
Aidha alilishauri Baraza la Sanaa Tanzania(Basata)kuwaangalia
wasanii wachanga ambao wanachipukia ili waweze kuona umuhimu wa fani hiyo kwa
kupewa nafasi.
EmoticonEmoticon