NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
LIGI KUU Tanzania bara inaingia raundi
ya tisa leo kwa michezo mbalimbali ambayo itapigwa kwenye viwanja vya Mabatini, Mkwakwani,Azam Complex na Manungu Turian mkoani Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari,Ofisa Habari wa Shirikisho la soka hapa nchini TFF,Boniface Wambura amesema kwa mechi kati ya Ruvu Shooting na Rhino Rangers (Mabatini, Mlandizi),
Mgambo Shooting na Mbeya City (Mkwakwani, Tanga), Azam na JKT Ruvu (Azam
Complex, Dar es Salaam) na Mtibwa Sugar na Oljoro JKT (Manungu,
Turiani).
Alizitaja mechi
zitakazooneshwa moja kwa moja (live) na Azam TV kupitia TBC1 wikiendi
hii ni kati ya Simba na Tanzania Prisons itakayochezwa Jumamosi katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na ile kati ya Azam na JKT Ruvu
itakayofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Azam Complex.
EmoticonEmoticon