BI.SAKINA MWINYIMKUU: JENGENI UTAMADUNI WA UTENDAJI UNAOTEGEMEA MATOKEO

July 25, 2025 Add Comment


*Dodoma, Julai 25, 2025*  

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Bi. Sakina Mwinyimkuu, amewataka watumishi wa umma kutumia maarifa waliyopata katika mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini ili kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika kazi zao.

Akifunga rasmi mafunzo hayo ya siku tano yaliyofanyika jijini Dodoma, Bi. Sakina amesisitiza umuhimu wa kujenga utamaduni wa kazi bora unaozingatia matokeo (results-based performance), kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

> “Mafunzo haya si kwa manufaa yenu binafsi pekee, bali yatumike kama nyenzo ya kuleta mabadiliko chanya katika taasisi zenu, sambamba na kuendeleza maadili ya uwajibikaji,” amesema Bi. Sakina.

Ametoa rai kwa washiriki kuwa mabalozi wa kueneza uelewa huo kwa wengine katika maeneo yao ya kazi, ili kuimarisha utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia viwango vya kitaifa vya ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo.





BENKI YA CRDB YATOA MADAWATI 111 NA KUCHANGIA UJENZI WA UZIO SHULE YA SEKONDARI PROF. ADOLF MKENDA, ROMBO

July 25, 2025 Add Comment

 


Mkuu wa Wilaya Rombo, Raymond Mwangwala (watatu kulia) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Bank Foundation, Coletha Ndunguru (wapili kushoto) kwa ajili ya kuchangia ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa uzio wa Shule ya Sekondari Prof. Adolf Mkenda iliyopo wilayani Rombo katika Mkoa wa Kilimanjaro. Sambambama na hilo, pia Benki ya CRDB imekabidhi madawati 111 yenye thamani ya shilingi milioni 10, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kuchangia maendeleo ya jamii kupitia uwekezaji unaolenga sekta muhimu za afya, elimu na mazingira ambayo asilimia 1 ya faida baada ya kodi hutengwa kila mwaka kwa ajili ya kusaidia miradi ya kijamii yenye tija. Mchango huu unalenga kuhakikisha ushiriki wa Benki ya CRDB katika kukuza elimu na kuboresha mazingira ya kusomea yaliyo salama. Wengine pichani ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Cosmas Sadat (kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rombo, Emmanuel Sindiyo (kulia) pamoja na Afisa Tawala wa Rombo, Isack Martin.

Mkuu wa Wilaya Rombo, Raymond Mwangwala (kulia) akipokea moja ya madawati kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Bank Foundation, Coletha Ndunguru kwa ajili ya Shule ya Sekondari Prof. Adolf Mkenda iliyopo wilayani Rombo katika Mkoa wa Kilimanjaro. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Cosmas Sadat.
Mkuu wa Wilaya Rombo, Raymond Mwangwala akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi katika hafla hiyo, iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Prof. Adolf Mkenda iliyopo wilayani Rombo katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Bank Foundation, Coletha Ndunguru akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi katika hafla hiyo, iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Prof. Adolf Mkenda iliyopo wilayani Rombo katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Cosmas Sadat akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi katika hafla hiyo, iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Prof. Adolf Mkenda iliyopo wilayani Rombo katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Burudani pamoja na wanafunzi


Vipindi vya Miss Universe Tanzania 2025 Kuanza Leo, Fainali Agosti 23

July 25, 2025 Add Comment
Na Mwandishi Wetu

VIPINDI vya mashindano ya Miss Universe Tanzania 2025 vinatarajia kuanza kuonekana kuanzia leo Julai 25 mwaka huu katika king’amuzi cha Startimes Tanzania kupitia Chaneli yake ya ST Swahili lengo likiwa kuwapa nafasi Watanzania kuona matukio mbalimbali katika Miss Universe nchini.

MRADI WA SEQUIP KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU MKOANI SINGIDA-RC DENDEGO

July 25, 2025 Add Comment
Wananchi wametakiwa kushirikiana na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kulimda miundombinu ya shule iliyojengwa ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi mkoani Singida.