📌 *Yatolewa na Shirika la Offgridsun kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia*
📌 *Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia Wizara ya Nishati apongeza wadau kuunga mkono jitihada za Serikali*
📌 *Wananchi wapongeza*
Shirika la Offgridsun wakishirikiana na Shirika la Action for Community care leo tarehe 29 Julai 2025 wamegawa majiko banifu 310 kwa wananchi wa Kijiji cha Ndebwe wilayani Chamwino mkoani Dodoma ikiwa ni uungaji mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.
Valentina Quaranta ambaye ni Meneja wa Mradi kutoka Action for Community Care (ACC) amesema lengo wanalokusudia ni kugawa majiko banifu 200,000 kwa wananchi ambapo mpaka sasa wameshagawa majiko 25,000 kwa mkoa wa Tanga, Morogoro pamoja na Dodoma.
![]() |
Valentina Quaranta amesema majiko hayo banifu yanapunguza sana matumizi ya kuni na mkaa na hivyo kupunguza athari za uchafuzi wa mazingira.
Kwa upande wake, Nolasco Mlay, Mkurugenzi wa Nishati safi ya Kupikia kutoka Wizara ya Nishati amepongeza jitihada za wadau katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia.
Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha ifikapo 2034 asilimia 80 ya wananchi wanatumia Nishati Safi ya Kupikia. Hivyo amewaomba wadau hawa kufika na maeneo mengine ili kuongeza chachu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Ametoa wito kwa wananchi wa kijiji cha Ndembwe kuhakikisha
Wanayatunza majiko hayo ili kuendelea kulinda afya zao na mazingira kwa ujumla.
Wananchi wa kijiji cha Ndebwe kwa nyakatii tofauti wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita pamoja na wadau kwa kuwapatia majiko hayo ambapo wameahidi kuyatunza.
#NishatiTupokazini.
EmoticonEmoticon