Wananchi wametakiwa kushirikiana na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kulimda miundombinu ya shule iliyojengwa ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi mkoani Singida.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Halima Dendego wakati akizungumzia tathmini na hali ya elimu leo tarehe 25 Julai 2025 ambapo amesema kuwa uongozi wa mkoa huo umejipanga kuimarisha sekta ya elimu kufuatia maboresho makubwa yanayofanywa ikiwemo ujenzi wa shule mpya.
Rc Dendego amesema kuwa jumla ya shule 30 za kata zimejengwa kupitia Mradi wa kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari nchini (SEQUIP) sambamba na ujenzi wa shule mpya 1 ya wasichana ya Solya iliyopo wilayani Manyoni na Ujenzi wa shule 2 mpya za Amali ya Kitukutu iliyojengwa wilayani Iramba pamoja na Unyambwa iliyojengwa katika Manispaa ya Singida.
Ameongeza kuwa baada ya ujenzi wa shule hizo mkoa wa Singida umeongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne kutoka asilimia 87 mwaka 2021 hadi asilimia 93 mwaka 2024.
Mhe Dendego amebainisha kuwa Mkoa wa Singida katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 umepokea kiasi cha shilingi 25,058,738,146.
Hata hivyo mradi huo wa SEQUIP katika mkoa wa Singida pia umeongeza idadi ya wanafunzi wa kike wanaosoma masomo ya Sayansi kwa kukamilika kwa shule ya wasichana ya Solya ambayo imejengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.5.
Tangu mwaka 2021 mpaka sasa jumla ya shule mpya za kata 30 zimejengwa katika mkoa wa Singida, Ujenzi wa shule ya wasichana Solya iliyopo wilaya ya Manyoni, na ujenzi wa shule 2 za Amali za mkoa ambazo ni shule ya Amali ya Unyambwa iliyopo Manispaa ya Singida na ujenzi wa shule ya Amali ya Kitukutu iliyopo Wilayani Iramba.



EmoticonEmoticon