MAFUTA GHAFI MRADI WA EACOP KUZALISHA UMEME KUKIDHI MAHITAJI WAKATI WA DHARURA

July 21, 2025


*📌Mradi kutumia Megawati 100 za umeme wa TANESCO kama chanzo kikuu cha kuendeshea miundombinu.


*📌 Kazi ya utandazaji nyaya za umeme ardhini kipande namba 15 kilichopo Handeni yafikia asilimia 45*


*📌 Mradi wanufaisha Wazawa kupitia uhaulishaji wa teknolojia kutoka kwa Wataalamu toka nje*


Na Neema Mbuja, Tanga


Mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga utazalisha umeme wake kwa kutumia mafuta yatakayozalishwa ili kukidhi mahitaji ya umeme nyakati za dharura.

Hayo yamesemwa Mratibu wa Kipande namba 15 kwenye eneo la uchomeleaji, ulazaji  wa mabomba na utandazaji wa nyaya za umeme zitakazotumika kwa ajili ya vituo vya kusukuma mafuta, Mhandisi Peter Mwinuka wakati alipokuwa akizungumzia maandalizi ya ujenzi na utandazaji wa miundombinu kwa ajili ya uzalishaji wa umeme kwenye eneo la mradi ili kukidhi mahitaji ya dharura wakati wa utekelezaji wa mradi.

Amesema licha ya ujenzi wa miundombinu hiyo ya umeme wa dharura, Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania-(TANESCO),  linatarajia kuipatia EACOP jumla ya megawati 100 kwa ajili ya matumizi ya umeme kwenye eneo lote la mradi  kutoka vituo vya kupoza umeme vya Majani mapana, Kyaka, Kibeta, Bulyanhulu, Lusu,  na Singida, ambapo kwa upande wa Umeme wa majenereta utakaozalishwa utatumia vituo vya Muleba, Igungai,Mbogwe, Singida na Tanga  ambapo kila moja itakuwa na megawati 25.

Akizungumzia teknolojia hiyo ya uzalishaji umeme inavyofanya kazi, Mhandisi Peter amesema kimsingi mafuta yatasafirishwa sambamba na laini 2 kutoka tilenga hadi Uganda kwa kutumia majenereta maalumu kama ilivyo kwa njia ya gridi kwa kutumia laini maalumu zizlizo sambamba na bomba la mafuta.

Amesema kwa sasa kazi ya utandazaji miundombinu hiyo ya umeme sambama na bomba imefikia asilimia 45 na kuongeza kuwa vyanzo vingine vya umeme vitakavyotumika wakati wa utekelezaji wa mradi huo ni pamoja na umeme wa jua ambapo kwa sasa wako kwenye mazungumzo juu ya utekelezaji wa mradi huo ambao utatekelezwa eneo la kambi pindi mradi utakapokamilika

Amesema kwa mujibu wa mpango kazi, wanalazimika kulaza mabomba hayo kwa takribani kilometa 3 kwa siku kama hakuna changamoto. hadi kilomita 2 mpaka 1.5 kama kuna changamoto.

Akitoa tathmini ya ushiriki wa wazawa kwenye utekelezaji wa mradi wa EACOP sambamba na manufaa kwa wazawa mmoja wa wanufaika wa mradi ambaye ni kijana David Chinanda amesena kumekuwa na mafanikio makubwa kwenye mradi huo kutokana na ujuzi kutoka kwa wataalamu kutoka nje ya nchi ambao wana uzoefu mkubwa kwenye utekelezaji wa miradi kama hiyo.

Amesema hapo awali alikuwa hafahamu masuala mengi kuhusu ubora na utekelezaji wa miradi kwenye sekta ya mafuta ila kutokana na wataalamu wa nje kuwapa elimu ya ndani yeye amekuwa ni mjuzi zaidi kiasi cha kuwafundisha wengine

‘’ Kiukweli mimi sikuwa mtaalamu kabisa kwenye hii teknolojia ya kusimika mabomba ardhini ila nawashukiru hawa wataalamu kwa sasa wazawa tumenufaika na utaalamu wao na tunaweza kufanya kazi popote hata za kimataifa’’ Amesema David.

Ameeleza kuwa, mradi huo wa Bomba la Mafuta Ghafi umeajiri vijana wengi wenye ujuzi na wasio na ujuzi na wamekuwa wakifanya vizuri kitaaluma.

Kwa upande wake mtaalamu wa masuala ya ubora na ambaye ni msimamizi wa mradi wa kipande namba 15, Mhandisi Gokhan Demircan amesema anafurahishwa na namna wazawa wanaotekeleza mradi wa EACOP wanavyojifunza kwa bidii teknolojia mbalimbali na kufanya vizuri.

Amesema vijana wengi wazawa walioko kwenye mradi wa EACOP wanaweza kuutumia ujuzi huo kwenye utekelezaji wa miradi minhine mikubwa ndani na nje ya nchi kwa kuwa ujuzi walioupata ni zaidi ya ule wa vyuo vya _mafunzo.



Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »