Vipindi vya Miss Universe Tanzania 2025 Kuanza Leo, Fainali Agosti 23

July 25, 2025 Add Comment
Na Mwandishi Wetu

VIPINDI vya mashindano ya Miss Universe Tanzania 2025 vinatarajia kuanza kuonekana kuanzia leo Julai 25 mwaka huu katika king’amuzi cha Startimes Tanzania kupitia Chaneli yake ya ST Swahili lengo likiwa kuwapa nafasi Watanzania kuona matukio mbalimbali katika Miss Universe nchini.

MRADI WA SEQUIP KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU MKOANI SINGIDA-RC DENDEGO

July 25, 2025 Add Comment
Wananchi wametakiwa kushirikiana na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kulimda miundombinu ya shule iliyojengwa ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi mkoani Singida.

BIL 36.596 ZA MRADI WA SEQUIP ZILIVYO INUFAISHA DODOMA KWENYE SEKTA YA ELIMU

July 24, 2025 Add Comment
Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa maeneo ambayo yamepata fedha nyingi kupitia mradi wa kuimarisha ubora wa Elimu ya sekondari nchini SEQUIP ambapo umepokea zaidi ya Bilioni 36.596.

DKT.BITEKO ATOA WITO VYOMBO VYA HABARI KUELIMISHA JAMII KUHUSU MASHUJAA

July 24, 2025 Add Comment

📌Rais Samia mgeni rasmi Maadhimisho ya Mashujaa kesho


📌Atoa wito kwa wananchi kushiriki Maadhimisho ya Mashujaa


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa vyombo vya habari kushirikiana na Serikali katika kuelimisha jamii kuhusu historia ya mashujaa nchini.


Dkt. Biteko ametoa wito huo Julai 24, 2025 katika Uwanja na Mnara wa Mashujaa uliopo Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kukagua maadalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa.

“ Ninatoa wito kwa wananchi wote kushiriki kwa wingi kwenye tukio hili adhimu. Hii ni siku yetu sote, siku ya kumkumbuka Mtanzania mwenzetu aliyesimama kwa ajili ya Taifa. Vivyo hivyo, nawaomba nyinyi waandishi wa habari, pamoja na vyombo vyenu na pia mitandao ya kijamii mshirikiane na Serikali katika kuelimisha jamii kuhusu historia ya mashujaa wetu, thamani ya mchango wao, na sababu ya sisi kuendelea kuwakumbuka kila mwaka,” amesema Dkt. Biteko.

Amezungumzia maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa na kusema kuwa yanaendelea vizuri na mgeni rasmi katika tukio hilo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, huku akisisitiza kuwa siku hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwakumbuka, kuwaenzi na kuwaheshimu mashujaa wetu waliotoa maisha yao, nguvu zao, na sadaka zao kwa ajili ya uhuru, amani na maendeleo ya Taifa.



Amefafanua kuwa kwa heshima hiyo, saa 6:00 usiku wa tarehe 24 Julai, 2025 siku moja kabla ya kilele cha maadhimisho, Mwenge wa Kumbukumbu ya Mashujaa utawashwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule kwa niaba ya Rais kuashiria kuanza kwa maombolezo ya Mashujaa wetu. 



Ameongeza kuwa katika siku ya maadhimisho kesho tarehe 25 Julai, 2025 kuanzia saa 3:00 asubuhi kutakuwa na gwaride rasmi la heshima litakalofanywa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama. Aidha, saa 6:00 usiku wa tarehe hiyohiyo mwenge wa Kumbukumbu ya Mashujaa utazimwa rasmi kuashiria hitimisho la maombolezo ya kumbukumbu Mashujaa kwa mwaka 2025.


Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa hufanyika kila mwaka tarehe 25 Julai 2025 kwa lengo la kuwakumbuka mashujaa waliopoteza maisha yao katika uwanja wa vita, waliostaafu baada ya kulitumikia Taifa kwa uaminifu, na wale waliopata majeraha katika kuilinda nchi yetu.



Mwisho.

SERIKALI YAZINDUA NYARAKA ZA USIMAMIZI WA MAAFA WILAYA SUMBAWANGA

July 24, 2025 Add Comment


Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na UNDP, imezindua nyaraka tatu muhimu za usimamizi wa maafa katika Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.


✅ Nyaraka zilizozinduliwa:


Mpango wa Kujiandaa na kukabiliana na maafa ya Wilaya (D-EPRP)


Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya Maafa (D-DRRS)


Ripoti ya Tathmini ya Vihatarishi, Uwezekano wa Kutokea na Uwezo wa kukbailian na maafa (RVCA)



📅 Uzinduzi umefanyika tarehe 23 Julai 2025 na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo na wananchi.

🎙️ Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Nyakia Chirukile:


> "Hii ni hatua muhimu kujenga mfumo wa utayari dhidi ya majanga kama mafuriko."



🎙️ Brigedia Jenerali (Mstaafu) Hosea Ndagalla, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa OWM:


> "Ni utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya 2022."



🎙️ UNDP Tanzania kupitia Bw. Godfrey Mulisa:


> "Mpango huu ni sehemu ya kusaidia jamii kujenga upya maisha yao na kuwa imara zaidi."

💬 Wadau wa maendeleo wametoa pongezi na kuahidi kushiriki kikamilifu kutekeleza mpango huu.



🟢 #Maafa2025 #Sumbawanga #UtayariDhidiYaMajanga #UNDP #OWM