ZAHARA MICHUZI ,ALIYEKUWA DED MEATU,IFAKARA NA GEITA AJITOSA MBIO ZA UBUNGE VITI MAALUMu UWT TABORA

June 30, 2025 Add Comment


Zahara Michuzi, mmoja wa watumishi wa umma waliopitia majukumu makubwa serikalini kwa miaka kadhaa, amejiunga rasmi katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Tabora.


Katika tukio lililosubiriwa kwa bashasha na matumaini makubwa, Zahara alipokea rasmi fomu ya kugombea kutoka kwa Katibu wa UWT wa Mkoa, Bi. Rhoda Sanga. Tukio hilo limezua msisimko miongoni mwa wanachama wa UWT, huku wengi wakimtaja Zahara kama mwanamke shupavu na mchapakazi mwenye historia isiyo na doa katika utumishi wa umma.

Zahara, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji (DED) katika Halmashauri tatu tofauti — Meatu (Simiyu), Ifakara (Morogoro), na Geita (Geita Mjini) — anajivunia rekodi ya uongozi ulioleta mabadiliko halisi katika maeneo aliyohudumu. Kabla ya kupandishwa cheo kuwa DED, aliwahi pia kuwa Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) katika Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, nafasi aliyoitumikia kwa weledi na kujenga imani kwa viongozi na wananchi.


Kwa kuingia kwake kwenye siasa, hasa katika nafasi ya uwakilishi wa wanawake kupitia UWT, Zahara analeta pamoja uzoefu wa kiutawala, usimamizi wa miradi ya maendeleo, na uelewa wa changamoto halisi zinazowakabili wanawake na jamii kwa ujumla katika mkoa wa Tabora na Tanzania nzima.



Wadadisi wa siasa wanaona uamuzi wa Zahara kama hatua ya kuhamasisha wanawake waliobobea katika sekta ya umma kushiriki moja kwa moja katika uundaji wa sera, hasa zile zinazolenga ustawi wa wanawake, vijana, na makundi maalum.

SALEHE MHANDO ACHUKUA FOMU KUGOMBEA JIMBO LA KILINDI MKOANI TANGA

June 30, 2025 Add Comment


 Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika na Mkuu wa Utawala Ofisi ndogo ya CCM Makao Makuu Lumumba jijini Dar Es Salaam, Ndugu Salehe Mbwana Muhando, leo Jumatatu Juni 30,2025 amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kilindi,mkoani Tanga,kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao.





MCHENGERWA AOMBA RIDHAA KWA CCM KUGOMBEA UBUNGE WA RUFIJI

June 30, 2025 Add Comment

Na Mwandishi Wetu - Rufiji

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI na aliyekuwa Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Juni 30, amejitokeza kuomba ridhaa kwa Chama chake- Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchaguliwa kuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu.

MJUE MTOTO WA MFANYABIASHARA MAARUFU SEIF SAID MWERA ANAYETAJWA KUGOMBEA JIMBO LA TEMEKE

June 29, 2025 Add Comment


Seif Said Mwera alikuwa ni miongoni mwa waasisi wa Biashara ya Usafirisha wa Abiria kusini Mwa Tanzania ambapo Ma BUS yake yalikuwa yakisafiri kutoka Dar Es Salaam kuelekea Mloka kwa Kipindi cha Takriban miongo 4 toka miaka ya Sabini. 

Pamoja na Mwera, majina mengine maarufu ya wakati ule katika sekta ya usafirisha yalikuwa Akida, Manitu na Born Coast, hawa ni miongoni mwa Matajiri wa Kwanza kutokea katika eneo la Temeke na Ukanda Wa Kusini Mwa Tanzania. 



Jina la Mwera ni jina Maarufu katika Wilaya ya Temeke na Kusini na Mwa Tanzania.Mwera, alikuwa Mzalendo mwenye kupenda Nchi yake na watu wa Nyumbani kwake, kiasi cha kuita Ma BUS yake kuyaita MZALENDO BUS SERVICE. 



Uzalendo wake ulidhihirika zaidi pale wakati wa Vita vya Tanzania na Uganda ambapo alijitolea Bus lake kwenda kusaidia katika Vita vya Tanzania na Uganda Mwaka 1979.



Sambamba na hilo, Mwera ndie aliyekuwa MKANDARASI wa Ujenzi wa Shule zote za Rufiji, wakati wa utengenezaji wa Vijiji vya Ujamaa Mwaka 1972, ambapo Watu wa Rufiji walihama kutoka katika Vijiji vya Mabondeni kuja katika Vijiji vya Juu. 



Mwera pia alikuwa, mdau Mkubwa wa Maendeleo katika Wilaya ya Rufiji na Temeke Dar Es Salaam ambako alikuwa akiishi katika maisha yake yote.



Mwera, amechangia uimara, uanzishwaji na Ustawi wa Umoja wa Maendeleo Rufiji kwa kifupi (UMAKURU).



Umoja ambao ulileta mwamko katika Ujenzi wa Shule za Secondary ndani ya Wilaya ya Rufiji, ambapo vijana wengi walipata nafasi ya kusoma katika shule hizo.



Kwa ujumla alikuwa Mdau Mkubwa wa Maendeleo katika maeneo mbali mbali alichangia ujenzi wa Misikiti, ukiwemo Msikiti wa Temeke Mwisho, alichangia Ujenzi wa Ofisi za CCM ikiwemo ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Miburani kabla ya kuzaliwa kwa  Kata ya Mtoni.



Seif Said Mwera,  alizaliwa Mwaka 1934 katika Kijiji cha Mgoholi ambacho kwa sasa kinaitwa Kipo katika Wilaya ya Rufiji, na kufariki Mwaka 2001 jijini Dar Es Salaam.



Allah aendelee kumpuzisha kwa amani Mwanawe Tano Seif Mwera anayetajwa kugombea Ubunge katika Jimbo la Temeke amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega na Kalambo kwa nyakati tofauti. 


Ametumikia nafasi ya Ukuu wa Wilaya kwa miaka Saba. Aidha Tano anafahamika kwa utendaji mahili ulitukuka ambapo alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega aliweza kusimamia utekelezaji wa miradi mbali mbali kwa ufanisi mkubwa.



Msimamizi wa Ujenzi wa Vituo vya Afya Nasa, Igalukilo na Hospital ya Wilaya ya Busega. Miradi ya Maji, Lamadi, Nyashimo na Kiloleli.



Alifanya Harambee kubwa uliyo wezesha ujenzi wa Shule Tatu mpya za secondary, Shule ya Secondary Dr Chegeni, Antony Mtaka na Nyamikoma.



Alisimamia kikamilifu mapambano dhidi ya Uvivu haramu. Alisimamia kikamilifu shughuli za Kilimo na Utalii kutaja kwa Uchache. 



Alipokuwa katika Wilaya ya Kalambo alileta mapinduzi makubwa ya Ujenzi wa Miradi ya maendeleo kama Vituo vya Afya, madarasa n.k. Tano alipiga marufuku ujenzi wa kutumia matofali ya kuchoma na matope badala yake matumizi ya tofauli za Block kuimarishwa na kuleta mapinduzi makubwa katika Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa. 



Tano pia anafahamika kwa umahili wake wa kupenda Maendeleo ya Wanawake ambapo ameanzisha Taasisi ya Wanawake Lakimoja yenye lengo la kuunganisha Wanawake kupinga ukatili wa Kijinsia na Umasikini.



Mtandao ambao umeleta hamasa kubwa kwa Wanawake kushiriki shughuli za kiuchumi na kuepuka ukatili wa Kijinsia.Kikubwa Tano, anachojivunia ni huasisi wa Ujenzi  wa Shule ya Secondary Bi Titi Mohammed iliyopo Rufiji katika Kijiji cha Kilimani ambayo kwa sasa inaitwa shule ya Secondary Ujamaa.



Tano alifanya Harambee kubwa katika Ukumbi wa PTA kuhakikisha shule hiyo inapata michango na msukumo  wa kujengwa.



Kwa ujumla Tano ni Kiongozi mkweli, mwaminifu, mpenda maendeleo, mbunifu, hodari wa kazi, ana elimu nzuri, uzoefu wa uongozi , ana upeo mkubwa kuhusu maendeleo ya uchumi, jamii na ujenzi wa Taifa kwa ujumla. 

Karibu Temeke Tano Seif Mwera.

DKT.BITEKO AWASILI RWANDA KUSHIRIKI MKUTANO WA NYUKLIA AFRIKA

June 29, 2025 Add Comment


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt Doto Biteko Juni 29, 2025 amewasili Kigali nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano unaohusu masuala ya nyuklia Afrika.

Katika Mkutano huo unaotarajiwa kuanza Juni 30 hadi Julai 1, 2025  nchini humo unajumuisha wadau wa nishati kutoka ndani na nje ya Afrika wenye lengo la  kuharakisha  matumizi ya nyuklia kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuleta mabadiliko ya nishati Afrika.

Pamoja na ushiriki wake katika Mkutano huo Dkt. Biteko anatarajiwa kufungua mjadala wenye mada kuhusu nishati Afrika na utashi wa kisiasa.


Aidha, katika Mkutano huo Dkt. Biteko ameambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na Mkurugenzi wa Tume ya Mionzi ya Atomiki, Prof. Najat Mohamed.




Mwisho