Seif Said Mwera alikuwa ni miongoni mwa waasisi wa Biashara ya Usafirisha wa Abiria kusini Mwa Tanzania ambapo Ma BUS yake yalikuwa yakisafiri kutoka Dar Es Salaam kuelekea Mloka kwa Kipindi cha Takriban miongo 4 toka miaka ya Sabini.
Pamoja na Mwera, majina mengine maarufu ya wakati ule katika sekta ya usafirisha yalikuwa Akida, Manitu na Born Coast, hawa ni miongoni mwa Matajiri wa Kwanza kutokea katika eneo la Temeke na Ukanda Wa Kusini Mwa Tanzania.
Jina la Mwera ni jina Maarufu katika Wilaya ya Temeke na Kusini na Mwa Tanzania.Mwera, alikuwa Mzalendo mwenye kupenda Nchi yake na watu wa Nyumbani kwake, kiasi cha kuita Ma BUS yake kuyaita MZALENDO BUS SERVICE.
Uzalendo wake ulidhihirika zaidi pale wakati wa Vita vya Tanzania na Uganda ambapo alijitolea Bus lake kwenda kusaidia katika Vita vya Tanzania na Uganda Mwaka 1979.
Sambamba na hilo, Mwera ndie aliyekuwa MKANDARASI wa Ujenzi wa Shule zote za Rufiji, wakati wa utengenezaji wa Vijiji vya Ujamaa Mwaka 1972, ambapo Watu wa Rufiji walihama kutoka katika Vijiji vya Mabondeni kuja katika Vijiji vya Juu.
Mwera pia alikuwa, mdau Mkubwa wa Maendeleo katika Wilaya ya Rufiji na Temeke Dar Es Salaam ambako alikuwa akiishi katika maisha yake yote.
Mwera, amechangia uimara, uanzishwaji na Ustawi wa Umoja wa Maendeleo Rufiji kwa kifupi (UMAKURU).
Umoja ambao ulileta mwamko katika Ujenzi wa Shule za Secondary ndani ya Wilaya ya Rufiji, ambapo vijana wengi walipata nafasi ya kusoma katika shule hizo.
Kwa ujumla alikuwa Mdau Mkubwa wa Maendeleo katika maeneo mbali mbali alichangia ujenzi wa Misikiti, ukiwemo Msikiti wa Temeke Mwisho, alichangia Ujenzi wa Ofisi za CCM ikiwemo ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Miburani kabla ya kuzaliwa kwa Kata ya Mtoni.
Seif Said Mwera, alizaliwa Mwaka 1934 katika Kijiji cha Mgoholi ambacho kwa sasa kinaitwa Kipo katika Wilaya ya Rufiji, na kufariki Mwaka 2001 jijini Dar Es Salaam.
Allah aendelee kumpuzisha kwa amani Mwanawe Tano Seif Mwera anayetajwa kugombea Ubunge katika Jimbo la Temeke amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega na Kalambo kwa nyakati tofauti.
Ametumikia nafasi ya Ukuu wa Wilaya kwa miaka Saba. Aidha Tano anafahamika kwa utendaji mahili ulitukuka ambapo alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega aliweza kusimamia utekelezaji wa miradi mbali mbali kwa ufanisi mkubwa.
Msimamizi wa Ujenzi wa Vituo vya Afya Nasa, Igalukilo na Hospital ya Wilaya ya Busega. Miradi ya Maji, Lamadi, Nyashimo na Kiloleli.
Alifanya Harambee kubwa uliyo wezesha ujenzi wa Shule Tatu mpya za secondary, Shule ya Secondary Dr Chegeni, Antony Mtaka na Nyamikoma.
Alisimamia kikamilifu mapambano dhidi ya Uvivu haramu. Alisimamia kikamilifu shughuli za Kilimo na Utalii kutaja kwa Uchache.
Alipokuwa katika Wilaya ya Kalambo alileta mapinduzi makubwa ya Ujenzi wa Miradi ya maendeleo kama Vituo vya Afya, madarasa n.k. Tano alipiga marufuku ujenzi wa kutumia matofali ya kuchoma na matope badala yake matumizi ya tofauli za Block kuimarishwa na kuleta mapinduzi makubwa katika Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa.
Tano pia anafahamika kwa umahili wake wa kupenda Maendeleo ya Wanawake ambapo ameanzisha Taasisi ya Wanawake Lakimoja yenye lengo la kuunganisha Wanawake kupinga ukatili wa Kijinsia na Umasikini.
Mtandao ambao umeleta hamasa kubwa kwa Wanawake kushiriki shughuli za kiuchumi na kuepuka ukatili wa Kijinsia.Kikubwa Tano, anachojivunia ni huasisi wa Ujenzi wa Shule ya Secondary Bi Titi Mohammed iliyopo Rufiji katika Kijiji cha Kilimani ambayo kwa sasa inaitwa shule ya Secondary Ujamaa.
Tano alifanya Harambee kubwa katika Ukumbi wa PTA kuhakikisha shule hiyo inapata michango na msukumo wa kujengwa.
Kwa ujumla Tano ni Kiongozi mkweli, mwaminifu, mpenda maendeleo, mbunifu, hodari wa kazi, ana elimu nzuri, uzoefu wa uongozi , ana upeo mkubwa kuhusu maendeleo ya uchumi, jamii na ujenzi wa Taifa kwa ujumla.
Karibu Temeke Tano Seif Mwera.
EmoticonEmoticon