MCHENGERWA AOMBA RIDHAA KWA CCM KUGOMBEA UBUNGE WA RUFIJI

June 30, 2025

Na Mwandishi Wetu - Rufiji

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI na aliyekuwa Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Juni 30, amejitokeza kuomba ridhaa kwa Chama chake- Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchaguliwa kuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu.

Mhe. Mchengerwa amefika kwenye ofisi ya Wilaya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rufiji katika Mji wa Utete kilomita takribani 60 kutoka barabara kuu ya Dar es Salaam - Lindi kuchukua na kisha kukabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Rufiji na baada ya kukamilisha taratibu zote akairejesha.
Mhe. Mchengerwa aliambatana na mama yake mzazi, ambapo baada ya kuwasilisha fomu asema ameamua kutumia haki ya kuchagua na kuchaguliwa ili aendelee kuwaletea maendeleo wananchi wa Rufiji na kisha akaondoka.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »