Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

TUME YATANGAZA RATIBA YA VYAMA KUCHUKUA FOMU ZA WAGOMBEA WA URAIS

August 08, 2025 Add Comment


Na Mwandishi Wetu 

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza ratiba ya kuchukua fomu za uteuzi kwa wagombea wa vyama 14 vya siasa waliopendekezwa kugombea nafasi za Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaanza kesho tarehe 09 Agosti, 2025.


Mkurugenzi wa INEC, Ndugu, Kailima Ramadhani akizungumza jijini Dodoma leo tarehe 08 Agosti, 2025 amewataja wagombea watakaochukua fomu kesho tarehe 09 Agosti, 2025 kuwa ni kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), National Reconstruction Alliance (NRA) na Alliance for African Farmers Party (AAFP). 


“Hadi leo tarehe 08 Agosti, 2025, tumepokea barua kutoka katika vyama vya siasa kumi na nne (14) zikiainisha tarehe na muda ambao wanachama wa vyama vyao waliowapendekeza kugombea nafasi za Kiti cha Rais na Makamu wa Rais watafika ofisi za Tume zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma kwa ajili ya kuchukua Fomu za Uteuzi,” amesema Ndugu. Kailima.


Amevitaja vyama vingine na tarehe za wagombea kuchukua fomu kuwa ni pamoja na na Chama cha MAKINI tarehe 10 Agosti, 2025, The National League for Democracy (NLD) tarehe 10 Agosti, 2025, United Peoples’ Democratic Party (UPDP) tarehe 10 Agosti, 2025 na African Democratic Alliance Party (ADA – TADEA) tarehe 11 Agosti, 2025.


Vyama vingine ni Union for Multiparty Democracy (UMD) tarehe 11 Agosti, 2025, Tanzania Labour Party (TLP) tarehe 11 Agosti, 2025, Chama Cha Kijamii (CCK), tarehe 12 Agosti, 2025, Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), tarehe 12 Agosti, 2025, Alliance for Democratic Change (ADC), tarehe 12 Agosti, 2025, Democratic Party (DP) tarehe 13 Agosti, 2025 na National Convention for Construction and Reform (NCCR – MAGEUZI) tarehe 15 Agosti, 2025.


Ndugu Kailima amesema tayari Tume imeviandikia vyama hivyo vya siasa barua kuvijulisha kuhusu ratiba hiyo ya utoaji fomu za uteuzi.  


“Aidha, ni muhimu tukumbuke kuwa, ratiba hii inahusu vyama kumi na nne (14) pekee vilivyowasilisha taarifa hadi kufikia leo tarehe 08 Agosti, 2025, hivyo iwapo vyama vingine vitajitokeza, tutaandaa ratiba husika na kuwajulisha,” amesema. 


Amevipongeza vyama vyote vya siasa kwa kuendelea kufanya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 na kuongeza kuwa, Tume kwa upande wake itazingatia katiba, sheria na kanuni wakati wote wa mchakato wa uchaguzi. 


Mwisho.

ALIYEKUWA MENEJA WA KANDA YA MASHARIKI TMDA DAR ES SALAAM AMWANGUSHA MWIJAGE KURA ZA MAONI MULEBA KASKAZINI

August 05, 2025 Add Comment




Na Mariam Kaagenda _Kagera 

Adonis Bitegeko aliyekuwa Meneja  wa  TMDA  Kanda ya Mashariki ameshinda Uchaguzi wa Kura za maoni Jimbo la Muleba Kasikazini katika Uchaguzi wa ndani wa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya Ubunge  kwa kupata Kura 4392 na kumshinda aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo  Charles Mwijage ambaye amepata Kura 2320 

JUDITH KAPINGA AIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI JIMBO LA MBINGA VIJIJINI

August 05, 2025 Add Comment

 

JIMBO LA MBINGA VIJIJINI


1. JUDITH KAPINGA - 12,975

2. BENAYA KAPINGA - 1,292

3. JAMES MAPUNDA - 416

4. ALLEN MHAGAMA - 133

5. CPA MARTIN - 80

6. PHILIMON NKOLELA - 45

UMMY MWALIMU ASHINDA KURA ZA MAONI JIMBO LA TANGA MJINI

August 05, 2025 Add Comment



Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tanga Mjini wamemchagua ndugu. Ummy Ali Mwalimu kuwa mgombea ubunge wa Jimbo hilo kwa kura 5,750 kati ya kura 10,293 zilizopigwa.


Akitangaza matokeo hayo August 04, 2025 Msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa Jimbo la Tanga Mjini linajumla ya wajumbe 12,620 na waliopiga kura ni 10,293 ambapo kura zilizoharibika ni 117, kura halali zilizopigwa ni 10,176 sawa na Wastani wa asilimia 56.5


Ummy Ali Mwalimu amepata kura 5,750 ambayo ni sawa na 56.5%, Omary Ayoub akipata 4,146 sawa na 40%, Kassim Mbaraka 80 sawa na 1%, Rajabu Abasi 130 sawa na 1% huku Arif Fazel akipata kura 70 sawa na 0%.

DKT.BITEKO ASHIRIKI KUPIGA KURA ZA MAONI BUKOMBE GEITA

August 04, 2025 Add Comment

Mtia nia nafasi ya  ubunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Mashaka Biteko ashiriki kupiga kura za maoni kumchagua diwani wa  kata ya Bulangwa ambapo Msimamizi wa Uchaguzi ni Ndugu. Paskasi Mlagiri Mjumbe wa kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Bukombe, Agosti 4, 2025, Mkoani Geita.
 Dkt. Doto Mashaka Biteko Agosti 4, 2025 akiwa ukumbini pamoja na wajumbe wengine wa mkutano mkuu wa kata ya Bulangwa wakisikiliza maelekezo kutoka Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Wilaya, Ndugu. Paskasi Mlagiri kuelekea kupiga kura za maoni katika nafasi ya Udiwani na Ubunge Jimbo la Bukonbe, Mkoani Geita.
 Dkt. Doto Mashaka Biteko Agosti 4, 2025 akiwa ukumbini pamoja na wajumbe wengine wa mkutano mkuu wa kata ya Bulangwa wakisikiliza maelekezo kutoka Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Wilaya, Ndugu. Paskasi Mlagiri kuelekea kupiga kura za maoni katika nafasi ya Udiwani na Ubunge Jimbo la Bukonbe, Mkoani Geita.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Mashaka Biteko ashiriki kupiga kura za maoni kwa nafasi ya Ubunge na Udiwani katika kata ya Bulangwa ambapo Msimamizi wa Uchaguzi ni Ndugu. Paskasi Mlagiri Mjumbe wa kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Bukombe, Agosti 4, 2025, Mkoani Geita.