Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

OFISI YA KANDA YA KATI YATOA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MAABARA ZA KEMIA KWA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI DODOMA

September 30, 2025 Add Comment
Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Magdalena Mtenga (aliyesimama), akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usimamizi wa Maabara za Kemia kwa Wakuu wa Shule za Sekondari wa Jiji la Dodoma (TAHOSSA) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bustani, Wilaya ya Kondoa, Mkoa wa Dodoma, Septemba 29, 2025.

MRADI WA KIJANA TOGORA KUWANUFAISHA VIJANA ZAIDI YA 1000 JIJINI TANGA

September 30, 2025 Add Comment



Na Oscar Assenga, TANGA

MRADI wa Kijana Togora tunakusikiliza unaotekeleza na Taasisi ya Afya Cheki chini ya Programu ya Tanga Yetu unaofadhiliwa na Botnar Foundation na kusimamiwa na Innovex umezinduliwa rasmi Jijini Tanga huku vijana zaidi ya 1000 wenye umri wa miaka 11 hadi 35 kutoka Kata 27 wanatarajiwa kunufaika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika kwenye kituo cha Sayansi cha Stem Park Jijini humo, Mkurugenzi wa AfyaCheck na Msimamizi wa Mradi huo Dkt.Isaac Maro alisema kuwa mradi huo unalenga kusikiliza changamoto za maisha ya vijana Jijini Tanga kufuatia utafiti wa kina.

Mradi huo pia unalenga kusikiliza na kuwawezesha vijana kujadili kwa uwazi masuala yanayowagusa kwenye maeneo ya afya ya akili, afya ya uzazi na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na vilevi.

Alisema ujio wa mradi huo ni baada ya utafiti walioufanya uliyobainisha changamoto nyingi hivyo kuona ni vyema kuweka utaratibu maalum wa kuwasikiliza vijana ili kujua shida zao pamoja na kuona namna ya kuzitatua.

Mradi wa Kijana Togora, Tunakusikiliza unalenga kusikiliza na kuwawezesha vijana kujadili wazi masuala muhimu ya ya Afya ya akili afya ya uzazi na matumizi ya dawa za kulevya na vilevi.

Akizungumza kuhusu mradi huo Dkt Maro alielekeza pongezi nyingi kwa vijana wa Tanga jiji kwa kupewa jukwaa lakusikilizwa sauti zao na hatimae kuzitatua.

Awali akizungumza Mwakilishi wa Botner Foundation Dkt Hasan Mshinda ambao ndio wafadhili wa miradi ya Tanga yetu ikiwemo Kijana Togora alisema kuwa katika utafiti walioufanya waligundua matatizo mbalimbali ilikwemo mimba za utotoni, matumizi ya Madawa ya kulevya ambayo ndio hatarisha maisha ya vijana ambao ndio nguvu kazi Taifa.

Aidha alisema kuwa Mkoa wa Tanga upo kwenye ngazi ya juu kwa matumizi ya dawa za kulevya hivyo kupitia mpango huo wa kijana Togora tunakusikiliza watajua kwanini wanajihusisha matumizi hayo na kwamba watapa elimu ya jinsi ya kuachana uraibu huo ikiwemo ushirikiano katika ngazi ya familia .

Kwa Naye kwa upande wake, Mrakibu wa Polisi wilaya ya Tanga Keneth Muhangwa alisema Jeshi la polisi wameanzisha pia mradi wa ngorika kwa kuunga mkono juhudi hizo ili kutokomeza matumizi ya dawa ya kulevya hivyo kwani mara nyingi wao wamekuwa wakidili na matokeo ya mambo yanayotoke katika jamii.

Alisema kwamba wameona ni vyema wao Jeshi la Polisi kuwa mradi mahususi kwa kujadili utoaji wa elimu juu ya matumizi ya dawa za kulevya ambapo ni vyema kila kijana atoe ushirikiano ili kutimiza wajibu wake katika kutoa taarifa ya uhalifu na wahalifu badala ya kuhusika kuafanya uhalifu unaotokana matumizivya dawa ya kulevya.

Hata hivyo akizungumzia mradi huo Afisa Maendeleo Jiji la Tanga Fatma Kinyumbi ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo aliwashukuru na kuwapongeza Botner faundation kwa miradi mbalimbali inayohusu vijana chini ya Tanga yetu.


"Mradi wa kijana Togora ni mradi Muhimu sana kwa vijana hivyo manapaswa kuchangamkia fursa za elimu ili wafikie malengo yenu hususani kupitia mradi wa kijana Togora ni vyema kujitokeza kwa wingi ili kupata fursa inayotokana na mradi huo "alisema Kinyumbi



Mwisho.

NGORONGORO INATHAMINI MCHANGO WA WAONGOZA WATALII- NAIBU KAMISHNA MAKWATI

September 30, 2025 Add Comment


Na Mwandishi wa NCAA.

Karatu, Arusha.


Naibu Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Joas Makwati ameeleza kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) inathamini mchango wa waongoza watalii (Tour Guides) kwa kuwa kundi hilo ndio linalopokea wageni, kukaa nao mda mrefu na kuwaongoza maeneo mbalimbali ya hifadhi yenye vivutio vya Utalii hadi siku wanapondoka 

Akizungumza wakati wa Kilele cha tuzo za waongoza Watalii 2025 kilichofanyika tarehe 27 Septemba, 2025 Karatu ambapo Ngorongoro ni sehemu ya wadhamini wakuu, Makwati ameongeza kuwa waongoza watalii ni wadau wakubwa na na wamekuwa mabalozi wazuri wa vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro vikijumuisha Kreta ya Ngorongoro, Empakai, Olmot, Makumbusho ya Olduvai, mchanga unaohama, tambarare za Ndutu, wanyama wakubwa watano "Big Five" pamoja na vivutio vingine.

Ameongeza kuwa "Ngorongoro pamoja na shughuli za uhifadhi, inatunza utamaduni wa asili ikiwepo uhalisia wa chimbuko la binadamu wa kale, Nyayo za Laetoli, gunduzi mbalimbali za kihistoria, eneo lenye hadhi ya Jiopaki ambavyo vyote kwa pamoja vinafanya Ngorongoro kuwa kivutio bora cha utalii na moja ya Maajabu saba katika bara la Afrika" ameongeza Makwati.

 Kufanyika kwa tuzo za Waongoza Watalii Wilayani Karatu ni heshima ya  kuendela kuitangaza Ngorongoro kama kivutio bora za Utalii Afrika kwa wadau mbalimbali ndani na Nje ya Nchi.

Katika kilele cha tuzo hizo washindi wa mwaka huu ni Daudi Peter kutoka kampuni ya utalii ya “Gosheni Safari” aliyepata tuzo ya “Overall Best Tour Guide of the Year 2025” pamoja na Neema Amosi Ngowi (Singita) aliyepata tuzo ya “Best Female Tour Guide 2025”



TBN Yaingia MCT Rasmi: Mwenyekiti Asema Uanachama ni Njia ya Kulinda Weledi na Uhuru

September 29, 2025 Add Comment


























Na Mwandishi wetu

Tanzania Bloggers Network (TBN) imepiga hatua kubwa katika kutambulika rasmi baada ya kukabidhiwa hati za uanachama katika Mkutano Mkuu wa 27 wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), uliofanyika Septemba 25, 2025, jijini Dar es Salaam. TBN ilikuwa miongoni mwa wanachama wapya wanane (8) waliojiunga na Baraza.




Akizungumza baada ya makabidhiano, Mwenyekiti wa TBN, Ndugu Beda Msimbe, alisema kuna manufaa makubwa kwa wanablogu kujiunga na MCT.




"Uanachama huu unatoa uhalali na kutambuliwa rasmi kwa wanablogu mbele ya jamii, Serikali na wadau wengine. Tunajumuishwa katika familia kubwa ya vyombo vya habari vinavyojisimamia, na sasa wanablogu wanatambulika kama chanzo cha habari kinachowajibika," alisema Ndugu Msimbe.




Aliongeza kuwa, TBN sasa inafaidika na mfumo wa ulinzi wa Baraza, hasa katika masuala ya usuluhishi dhidi ya malalamiko. Alisisitiza kuwa mfumo huo utawalinda wanablogu kisheria na kiuchumi dhidi ya vitisho au uwezekano wa kufilisiwa kutokana na faini za kimahakama, kwa kuwa sasa wana kimbilio katika Kamati ya Maadili ya MCT.




Upanuzi huu unakwenda sambamba na wito uliotolewa na uongozi wa MCT unaosisitiza umuhimu wa mshikamano wa wanachama.




Katibu Mtendaji wa MCT, Bw. Ernest Sungura, alikumbusha kwamba kauli mbiu ya mkutano, “Uhai wa Wanachama ni Nguvu na Usalama wa Taaluma ya Habari,” inapaswa kuwa mwongozo.




"Ikumbukwe ni wanachama waliosema siku moja tujisimamie au lah tukubali kufa... Uhai wa wanachama upo katika kushiriki vikao na kulipa ada za uanachama," alisema Bw. Sungura, akionya kuwa enzi za kudhani wafadhili watatoa fedha kwa MCT zimekwisha, na hivyo uhai wa Baraza unategemea wanachama.




Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Ndugu Yusuf Khamis Yusuf, alisisitiza kuwa katika miaka hii 30 ya MCT tangu kuanzishwa kwake mwaka 1995, Baraza limejipambanua kama taasisi huru inayolinda weledi na maadili.




Weledi na Uhuru: Njia ya Baraka

Akifungua rasmi Mkutano huo, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo, Rais Mstaafu wa Nne wa Baraza, alisisitiza kuwa uwepo wa MCT umeokoa vyombo vingi vya habari kutokana na kufilisiwa.




Alisisitiza kuwa ni wajibu wa kila chombo cha habari, ikiwemo TBN, kuwa kiungo cha ukweli bila kuegemea upande mmoja. Alitahadharisha wanahabari akisema: "Kusimama kwenye haki ni kugumu kuliko kujipendekeza. Kusimama na haki kunahitaji sadaka. Siyo njia nyepesi au rahisi, lakini ni njia ya baraka mno na ni njia inayompendeza Mungu."




Jaji Mihayo pia alizindua rasmi Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT 2025) ambazo zitaendeshwa kwa mfumo wa kidijitali sambamba na tovuti mpya ya MCT, hatua inayodhihirisha dhamira ya Baraza kukuza weledi katika tasnia nzima.

WITO WATOLEWA KWA WADAU KUENDELEA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO ZA LISHE NCHINI

September 29, 2025 Add Comment

NA. MWANDISHI WETU - DAR ES SALAAM


Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Germana Leyna  ametoa wito kwa wadu wa masuala ya lishe nchini kuendelea kuunga mkono jitihada za kupambana na changamoto zinazokabili masuala ya Lishe huku akisema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukabili changamoto hizo kwa kuwa na mikakati madhubuti.

Wito huo umetolewa  leo 29 Septemba, 2025 kwenye mahojiano maalumu katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)  Jijini Dar es Salaam katika kuelekea kwenye Mkutano Mkuu wa 11 wa Wadau wa Masuala ya Lishe. 


"Serikali imeendelea kuweka mikakati mbalimabli ikiwemo kuendelea kutoa elimu kwa umma na kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa wa masuala ya lishe ili kuendelea kuwa na Taifa lenye watu wenye lishe bora na niseme apa kuwa wadau waje tunganishe nguvu katika kupambana na changamoto za maswala ya Lishe" amesema Dkt Germana Leyna. 

Pia ameongoza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inawafikia wazalishaji hasa wakulima wawapo  katika shughuli zao za  kilimo na kuhakikisha wanapata elimu ya lishe bora na umuhimu wa kutunza chakula cha matumizi ya nyumbani badala ya kuuza chote.


Ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wadau kuendelea kujitokeza na kuendelea kuweka chachu katika masuala ya lishe nchini.




=MWISHO=