📌Yasema utachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi.
📌Yasisitiza utekelezaji wa mpango huo kuleta matokeo Chanya kwa wananchi.
Na. Mwandishi wetu, Dar Es Salaam
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupitia Mpango wa Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya TANESCO na Benki ya CRDB, ukilenga kuwawezesha wananchi wa mijini na vijijini kupata huduma ya umeme kwa urahisi na kwa wakati, ili kuchochea fursa za maendeleo katika nyanja mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza leo, Novemba 23, 2026, Jijini Dar es Salaam, katika Kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mpango huo mbele ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi. Subira Mgalu amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za kutekeleza Mpango wa Misheni 300, unaolenga kuhakikisha hadi kufikia mwaka 2030 wananchi milioni 300 barani Afrika wanafikiwa na Nishati ya umeme.
Amesema jitihada hizo zilizofanywa na TANESCO kwa kushirikiana na Benki ya CRDB , kutasaidia wananchi kunufaika na utaratibu wa kugharamiwa gharama za uunganishaji wa umeme, hatua ambayo itaongeza kasi ya kuzifikia kaya takribani milioni 1.7 kwa mwaka, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Nishati.
“Ninaipongeza TANESCO na Benki ya CRDB kwa hatua hii muhimu ya kuanzisha ushirikiano unaolenga kumrahisishia mwananchi kupata huduma ya umeme Kwani Ushirikiano huu ni mfano bora wa namna taasisi za umma na sekta binafsi zinavyoweza kuunganisha nguvu na rasilimali ili kutatua changamoto kwa wananchi moja kwa moja,” amesema Bi. Subiria Mgalu.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amesema kupitia ushirikiano huo kati ya Serikali na sekta binafsi, ni hatua muhimu kwa serikali katika kuhakikisha ya wananchi wote wanaendelea kufikiwa na huduma ya umeme bila kikwazo chochote.
Amesema utekelezaji wa ushirikiano huo ni matokeo ya Serikali, chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuweka mazingira wezeshi ya kukuza fursa za kiuchumi na kijamii kupitia Nishati ya umeme.
“Mpango huu ni muhimu sana kwa Wananchi unarahisisha kuwasogezea huduma muhimu ya Umeme Kwani kupitia ushirikiano huu utatuwezesha angalau wa Tanzania milioni 1.7 kwa mwaka wanafikiwa na huduma ya Umeme ili kuhakikisha Tanzania mafia malengo ya Moango wa Misheni 300
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Abdulmajid Nsekela amesema benki hiyo ni mshirika wa maendelo hapa nchini na kuwekeza katika Nishati nikuwekeza katika mstakabali wa Uchumi kwa taifa kwani hatua hiyo inakwenda kuongeza watumiaji wa umeme hali itakayochochea ukuaji wa uchimi kwa wananchi.
Nao baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wamepongeza juu ya Mpango huo huku wakisema wanakwenda kuwa mabalozi Wazuri katika kuwahamasisha na kuwapa elimu Wananchi katika majimbo Yao.








EmoticonEmoticon