MAKAMU WA RAIS AKERWA NA UDANGANYIFU TANROADS MBEYA

October 17, 2026
Na Mwandishi Wetu,Mbeya

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Deogratius Ndejembi, amekerwa na uzembe na taarifa za kupotosha kuhusu ufunguaji wa barabara ya njia nne mkoani Mbeya, kuwapunguzia adha watumiaji wa barabara hiyo, baada ya kurejea kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika eneo la Kabwe.

Amechukizwa na kitendo cha Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga, kutoa maelezo ya kupotosha kuhusu kuanza kufungua barabara katika eneo la Mdope mkoani humo.

Akionesha kutoridhishwa na hali hiyo, leo alipofanya ziara ya kushutukiza akiwa Jijini Mbeya, Makamu wa Rais amehoji namna Serikali inavyotoa fedha nyingi bila kuona matokeo yanayolingana na thamani yake, akisisitiza kuwa shilingi bilioni 40 si fedha ndogo kiasi cha kuruhusu uzembe na usimamizi dhaifu.

Makamu wa Rais amemtaka Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, kuhakikisha hatua za uwajibikaji zinachukuliwa kuanzia kwa Meneja wa TANROADS aliyempatia taarifa zisizo sahihi, akisisitiza kuwa Serikali haitavumilia watendaji wanaowadanganya viongozi huku wananchi wakiendelea kupata adha ya miundombinu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »