MAFUNZO YA SDF YAMFUNGULIA FURSA ZA KIUCHUMI MWAMVUA ISSA HAMISI

October 25, 2026

Miaka minne baada ya kupata mafunzo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Mwamvua Issa Hamisi, mjasiriamali kutoka Kaliua, Tabora, ameendelea kukuza biashara yake ya uzalishaji na uchakataji wa bidhaa zitokanazo na mazao ya nyuki.

Mafanikio yake ni pamoja na kupata alama ya ubora wa bidhaa kutoka TBS, kusajili kampuni yake ya Mwamvua Food Processing kupitia BRELA, na kupata misimbo ya bidhaa (barcodes) kwa ajili ya utambulisho wa bidhaa zake sokoni.

Kupitia ujuzi alioupata, Mwamvua pia ameshiriki katika kukuza kikundi cha wanawake wachakataji wa mazao ya nyuki chenye wanachama 15. Kikundi hicho kilipata mkopo wa Sh milioni 10 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, ambao tayari umerejeshwa wote.

Aidha, amepanua fursa za masoko kupitia maonyesho ya wajasiriamali ndani na nje ya nchi, huku akiongeza aina za bidhaa zake kwa kujifunza kutengeneza sabuni, mishumaa na mafuta yatokanayo na mazao ya nyuki.

TEA inaendelea kuunga mkono maendeleo ya ujuzi na ujasiriamali kwa ajili ya kukuza fursa za kiuchumi na kujipatia kipato.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »