BARRICK BULYANHULU, CHRYSOS WAKABIDHI JENERETA SHULE YA MSINGI BUPAMBA

October 08, 2026

         

Vingozi wa Halmashauri ya Nyang'wale wakipokea msaada huo wa jenereta
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyang'wale Ntiriyo Ezekiel akiongea na wawakilishi wa Barrick Bulyanhulu na Chrysos Corporation ofisini kwake wakati wa hafla ya makabidhiano.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Bupamba katika picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Nyang'hwale na wawakilishi kutoka Barrick Bulyanhulu
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Bupamba katika picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Nyang'hwale na wawakilishi kutoka Barrick Bulyanhulu.

**
Barrick Bulyanhulu kwa kushirikiana na Kampuni ya Chrysos imekabidhi jenereta katika shule ya msingi Bupamba, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu na huduma za Shule.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwakilishi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Mary Lupamba ambaye ni Afisa Mahusiano ya Jamii, amesema msaada huo unalenga kuiwezesha shule kuwa na chanzo cha umeme cha uhakika, hivyo kusaidia shughuli mbalimbali za kitaaluma na kiutawala kuendelea kwa ufanisi.

“Tumeshirikiana na Chrysos kuunga mkono juhudi za serikali katika elimu kwa kutoa Jenereta hii ili walimu na wanafunzi waweze kufanya shughuli za masomo wakati wote hata kama umeme wa Tanesco ukikatika ",amesema Lupamba.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyang'wale Ntiriyo Ezekiel, ameushukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Chrysos Corporation kwa msaada huo, huku ukiahidi kuhakikisha jenereta hiyo inatunzwa na kutumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

Hatua hiyo inaendelea kuonesha dhamira ya kampuni hizo kushirikiana na Jamii zinazozunguka shughuli zao katika kuunga mkono maendeleo ya elimu na ustawi wa jamii.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »