WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Mei 28, 2026 amewasili kuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano la Kitaifa la Wadau wa Mazingira pamoja na maadhimisho ya miaka 40 ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) yanayofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Katika kongamano hilo, Dkt. Mwigulu ametembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya wadau wa mazingira na kupata fursa ya kujionea shughuli na teknolojia zinazotumika katika uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.
EmoticonEmoticon