TAASISI ZA USHINDANI AFRIKA ZATAKIWA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA UBADILISHANAJI UZOEFU

April 14, 2026
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, amesema kuwa mkutano wa taasisi za ushindani barani Afrika umeleta pamoja wadau muhimu kutoka nchi mbalimbali kwa lengo la kujadili changamoto zinazoikumba sekta ya biashara. 

Amesema mkutano huo unahusisha zaidi ya nchi 37 na unalenga kuimarisha ushirikiano miongoni mwa taasisi hizo.

Akizungumza katika mkutano huo, Londo alieleza kuwa moja ya malengo makuu ni kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo katika kusimamia ushindani wa kibiashara.

 Aidha, amesisitiza umuhimu wa kubadilishana mbinu na mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazofanana katika mataifa mbalimbali.

"Dunia ya sasa imekuwa kama kijiji, ambapo changamoto zinazotokea katika nchi moja huweza kuathiri nchi nyingine. Hivyo, mkutano huo ni fursa ya kujifunza na kupata suluhisho la pamoja kwa matatizo yanayoathiri biashara barani Afrika,"amesema
.
Londo amebainisha kuwa mabadiliko ya kiuchumi duniani, yakiwemo vita na kupanda kwa bei ya nishati, yameleta athari kubwa katika uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa. Hali hiyo imeongeza gharama za uzalishaji na kuathiri upatikanaji wa bidhaa na huduma.

Kutokana na hali hiyo, amesema kuwa kuna hatari ya kuongezeka kwa biashara zisizo halali, ambapo baadhi ya wafanyabiashara wanaweza kupunguza gharama kwa njia zisizozingatia ubora na usalama wa bidhaa.Hiyo inaleta changamoto kubwa kwa taasisi zinazosimamia ushindani.

Amesema taasisi hizo zina jukumu la kuhakikisha walaji wanalindwa na wanapata bidhaa bora kwa bei halali. Hata hivyo, amekiri kuwa changamoto za sasa zinahitaji mbinu mpya na ushirikiano wa karibu zaidi kati ya nchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC),Khadija  Ngasongwa amesema kuwa mkutano huo unahusisha pia wanachama binafsi zaidi ya 53 na taasisi za kikanda kama zile za Afrika Mashariki na COMESA. Lengo ni kuimarisha ushirikiano na kujenga uwezo wa pamoja.

Ameeleza kuwa kupitia jukwaa hilo, wataalamu wanapata nafasi ya kushirikiana katika masuala yenye athari za kuvuka mipaka (cross-border effects), ambapo changamoto ya nchi moja inaweza kuathiri nchi nyingine. Hivyo, ushirikiano ni muhimu katika kutatua matatizo hayo.

Kuna vikundi kazi vinavyoshughulikia maeneo mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu kwa walaji na uchunguzi wa vitendo vya ukiukwaji wa ushindani sokoni. Vikundi hivyI vina mchango mkubwa katika kuhakikisha soko linakuwa la haki,"amesema.

Akizungumzia kuhusu kupanda kwa bei, ameeleza kuwa si kila ongezeko husababishwa na udanganyifu wa wafanyabiashara, bali wakati mwingine hutokana na majanga ya asili au hali ya kimataifa. 

Amesema ni muhimu kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuchukua hatua, huku elimu kwa walaji ikiendelea kutolewa ili waweze kufanya maamuzi sahihi.

Naye Mwenyekiti wa AFC na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Ushindani Mauritius,Vipin Naugah amesema

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »