WAZIRI NDEJEMBI NA WAZIRI CHIKOTE WA ZAMBIA WAJADILI USHIRIKIANO SEKTA YA NISHATI

March 27, 2026


Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nishati wa Zambia, Mhe. Makozo Chikote, leo tarehe 27 Machi 2026 katika Jiji la Lusaka, Zambia.

Katika kikao hicho kilichowashirikisha wataalam kutoka nchi hizo mbili, Viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yaliyolenga kuimarisha na kuendeleza ushirikiano katika sekta ya nishati, hususan sekta ndogo ya mafuta na gesi.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio, Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Luteni Jeneral Mathew Edward Mkingule pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na taasisi zilizo chini yake.

Tanzania na Zambia zimekuwa na historia ya ushirikiano wa karibu katika sekta ya nishati, ikiwemo usimamizi na matumizi ya Bomba la Mafuta la TAZAMA, ambalo ni kiungo muhimu katika usafirishaji wa mafuta kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zambia.


Ushirikiano huo umeendelea kuchangia kuimarika kwa usalama wa nishati na kukuza uchumi wa nchi zote mbili.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »