SERIKALI YAONGEZA NGUVU KATIKA MIKAKATI YA KUHAKIKISHA UPATIKANAJI ENDELEVU WA MAFUTA NCHINI

March 28, 2026

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratias Ndejembi amekutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati  zinashughuliki mafuta na gesi nchini katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.


Kikao hicho kilichofanyika leo, tarehe 28 Machi 2026, ni sehemu ya juhudi za Serikali kuendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha usalama na upatikanaji wa mafuta.

Uhaba wa mafuta unaoshuhudiwa unatokana na changamoto za usambazaji katika soko la kimataifa, zilizochochewa na vita inayoendelea katika ukanda wa Mashariki ya Kati. 

Hali hiyo imeathiri njia muhimu za usafirishaji wa mafuta, ikiwemo kupungua kwa upitishaji wa shehena kupitia Mlango wa Bahari wa Hormuz, jambo lililosababisha kucheleweshwa kwa usafirishaji na hatimaye kupungua kwa upatikanaji wa mafuta katika baadhi ya maeneo.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio, Kamishna wa Mafuta na Gesi, Bw. Goodluck Shirima, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Mwainyekule, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Bw. Musa Makame, Mtendaji Mkuu wa PBPA Bw. Erasto Simon na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati kwa lengo la kupokea taarifa ya hali ya upatikanaji wa mafuta nchini.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »