MVUA YALETA ATHARI KWA KAYA 40 WILAYANI MKINGA KAMPUNI YA DUVII FARM YAWAFARIJI WAHANGA KWA KUTOA MISAADA

March 25, 2026

Na Oscar Assenga, MKINGA

MVUA kubwa iliyonjesha katika wilayani Mkinga mkoani Tanga imeleta athari kwa kata nne na kupelekea kaya 40 kupata madhara mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mali na makazi ya wananchi .

Kata ambazo zimekumbana na athari za mvua hizo ni Mtimbwani,Kwale,Doda na Manza

Kufuatilia hali hiyo wawekezaji wilayani humo wameanza kuwashika mkono wahanga hap kwa kutoa misaada mbalimbali ili kuweza kuwafariji ikiwemo Kampuni ya Duvii Farm ambao wamekabidhi misaada mbalimbali ikiwemo Mchele, Unga,Mafuta na sukari


Alisema kwamba msaada huo umefika wakati muafaka wakati wananchi hao waliokumbwa na changamoto hivyo waweze kupata ahueni kutoka na kadhia walioipata iliyotokana na mvua hizo.

“Kwa kiasi kikubwa mvua hizi zimeathiri kaya 40 ambapo pamoja na kuharibikiwa na makazi lakini chakula na mahitaji mengine viliathirika kwa kiwango kikubwa na hivyo msaada huo ni jambo kubwa.



“Tunamshukuru kwa sababu mmesikia kupitia vyombo vya habari baada ya RC kuwatembelea wahanga wa mafuriko hivyo msaada huu umekuja wakati muafaka “Alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Hata hivyo alisema kwamba baada ya kupokea msaada huo wataukabidhi kwa walengwa kwa sababu wanazo orodha ya wahanga hivyo watahakikisha wanawafikia walengwa ili waweza kutimiza malengo yaliyofikiwa.

Katika hatua nyengine aliwaoba wadau wengine waendelee kuwashika mkono kwa pamoja wataendelela kumarisha wilaya na kupitia kiwada chake ambacho kinaajiri wana mkinga kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kuweza kupata kipato.

Awali akizungumza Mwekezaji wa Kampuni ya Duvii Farm ya wilayani Mkinga Mkoani Tanga Said Duvi alisema kwamba wameamua kutoa msaada wa vitu mbalimbali ili kuwasaidia wananchi walioathirika na mafuriko ikiwa ni kuwashika mkono kutokana na madhara hayo.



Alisema kwamba walipokea taarifa ya kutokea maafa hayo na hivyo wao kama wawekezaji waliona ni vema kuwashika mkono waathirika wote waliopata maafa hayo.

Alisema kwamba kutokana na maafa hayo wamepoteza chakula,nyumba hivyo wameona watoe kidogo walichonacho ili kiweza kuwasaidia.

“Tumeleta Mchele,Unga,Mafuta na sukari lakini pia tutaendelea kuwasaidia kwa sababu matatizo ya maafa mtu aombei yanaweza kujitokeza muda wowote na sehemu yotote hivyo sisi kama wao wawekezaji wapo tayari kuwasaidia kwa hali na mali”Alisema

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »