MHE.MAKAMBA ASHIRIKi UFUNGUZI WA AWALI POWERINH AFRICAN SUMMIT LEO JIJINI WASHINGTON DC

March 19, 2026

 



Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Else Sia Kanza wameshiriki katika ufunguzi wa awali wa Powering African Summit leo, Machi 19, 2026 jijini Washington Dc.

Mkutano huu wa siku mbili unawakutanisha viongozi wa Serikali, wawekezaji na wadau wa sekta ya nishati kujadili mustakabali wa nishati barani Afrika, fursa za uwekezaji, pamoja na suluhisho endelevu kwa maendeleo ya sekta hiyo.

Katika mkutano huo, Naibu Waziri ameambatana na wataalam kutoka TANESCO, PURA pamoja na REA ambao watashiriki kwenye majadiliano kuhusu upatikanaji wa umeme kwa wote, uwekezaji katika ‘Energy Mix’ pamoja na usimamizi na maendeleo endelevu ya rasilimali za gesi na mafuta.




Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »