CHIEF WA KIBONDO MWANAMVUA RAJAB RUHAGA NYAMALIZA AFARIKI DUNIA GHALFA AKIWA MSIBANI MALINYI ,MOROGORO

March 25, 2026




Chief wa Kibondo mkoani Kigoma  Mama Mwamvua Rajab Ruhaga Nyamaliza amefariki dunia ghafla asubuhi ya tarehe 24 Machi 2026 akiwa msibani Malinyi, mkoani Morogoro.


Taarifa za kifamilia zinaeleza kuwa marehemu alikuwa amesafiri kwenda Malinyi kuhudhuria mazishi ya binti yake, Zubeda Juma Ruhaga, kabla ya kifo chake hicho cha kushtukiza kutokea.


Kifo hicho kimeacha simanzi kubwa kwa familia, ndugu, jamaa na wakazi wa Kibondo, ambako marehemu alikuwa akihudumu kama kiongozi wa kimila na mshauri muhimu wa jamii.


Kwa sasa, familia ipo katika maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Morogoro kuelekea Kibondo, Kigoma, kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika nyumbani kwake.


Taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi zinatarajiwa kutolewa na familia kadri mipango inavyoendelea.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »