Ujumbe wa kitaalamu kutoka Burkina Faso uliokuja kujifunza mifumo na mbinu bora za uendeshaji wa sekta ya madini nchini katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Barrick na Wizara ya Madini baada ya kutembelea mgodi wa Barrick Buzwagi. 
Meneja wa ufungaji wa mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastraal Mumbi akitoa maelezo ya maendeleo ya mchakato wa ufungaji wa mgodi kwa ujumbe wa kitaalamu kutoka Burkina Faso uliokuja kujifunza mifumo na mbinu bora za uendeshaji wa sekta ya madini nchini ulipotembelea eneo hilo.
Ujumbe wa kitaalamu kutoka Burkina Faso uliokuja kujifunza mifumo na mbinu bora za uendeshaji wa sekta ya madini nchini ukiangalia mandhari ya kongani ya Buzwagi.

Ujumbe wa kitaalamu kutoka Burkina Faso uliokuja kujifunza mifumo na mbinu bora za uendeshaji wa sekta ya madini nchini ukimsikiliza Meneja wa ufungaji wa mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastraal Mumbi ulipotembelea mgodi huo ambao uko katika mchakato wa kufungwa.
Ujumbe wa kitaalamu kutoka Burkina Faso uliokuja kujifunza mifumo na mbinu bora za uendeshaji wa sekta ya madini nchini ukimsikiliza Meneja wa ufungaji wa mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastraal Mumbi ulipotembelea mgodi huo ambao uko katika mchakato wa kufungwa.
Ujumbe wa kitaalamu kutoka Burkina Faso uliokuja kujifunza mifumo na mbinu bora za uendeshaji wa sekta ya madini nchini ukimsikiliza Meneja wa ufungaji wa mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastraal Mumbi ulipotembelea mgodi huo ambao uko katika mchakato wa kufungwa.
**
Wataalamu wa madini kutoka Burkina Faso watembelea Barrick Buzwagi na kupongeza ufungaji wa mgodi kwa viwango vya kimataifa
Ujumbe wa kitaalamu kutoka Burkina Faso uliokuja kujifunza mifumo na mbinu bora za uendeshaji wa sekta ya madini unaofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini, umetembelea Mgodi wa Barrick Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa na kupongeza mchakato wa ufungaji wa mgodi huo kwa viwango vya kimataifa unaozingatia utunzaji wa mazingira.
Ukiwa mgodini hapo ujumbe huo umetembelea maeneo mbalimbali ambayo kwa sasa yana mandhari ya kuvutia na mazingira bora na endelevu ambayo yataendelea kuleta manufaa kwa jamii inayozunguka eneo hili na wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika kongani ya Buzwagi Special Economic Zone, ambayo tayari imeishaanza kuwa na mwekeleo kwa kuwa kitovu cha biashara katika mikoa ya kanda ya ziwa na nchi jirani na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Meneja wa ufungaji wa mgodi huo, Mhandisi Zonnastraal Mumbi, amesema Barrick itaendelea kushirikiana na Serikali wakati wote kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa viwango vya kimataifa na kuwa mfano wa kuigwa kwa kufunga shughuli za mgodi na kuacha eneo lililokuwa mgodi linakuwa na miradi endelevu ya kuwanufaisha Wananchi na taifa kwa ujumla.
“Jukumu la Kampuni endelevu ya uchimbaji madini si kutengeneza thamani kwa wadau wakati uliopo bali pia ni kuhakikisha kuwa inaacha urithi mzuri ambao utaendelea kuhudumia jamii kwa muda mrefu baada ya uchimbaji kufikia mwisho katika mgodi wa Barrick Buzwagi”,amesema Mumbi.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Ujumbe huo, Halidou Ouedraogo amesema Burkina Faso imevutiwa na hatua za Tanzania katika kuimarisha uwazi na uwajibikaji, kuanzisha mifumo ya kusaidia wachimbaji wadogo kuingia katika uchimbaji rasmi, na kuunganisha Sekta ya Madini na maendeleo ya uchumi wa ndani. Aliongeza kuwa ziara hiyo inalenga kujifunza kwa vitendo ili kuboresha Sera, mifumo ya usimamizi, na mikakati ya maendeleo ya Sekta ya Madini nchini Burkina Faso.
Halidou Ouedraogo,amesema ufungaji wa mgodi huo umefanyika kwa weredi mkubwa na Barrick imeacha alama ya kudumu ambayo itakumbukwa mpaka vizazi vijavyo hasa kutokana na eneo hilo kutangazwa na Serikali kuwa kongani ya viwanda.
Katika kuboresha zaidi eneo hilo kibiashara kampuni ya Barrick imejenga jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege Uwanja wa Ndege wa Mgodi uliofungwa wa Buzwagi lenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya abiria 200 kwa wakati mmoja ikilinganishwa na abiria 25 tu hapo awali na tayari limekabidhiwa kwa Serikali.
Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi ulikuwa kitovu cha uchumi wa mkoa wa Shinyanga nchini Tanzania kwa takribani miaka 15 ambapo katika kilele chake, Buzwagi ulikuwa mgodi wa pili kwa ukubwa nchini Tanzania na uliajiri watu 3,000 na maisha yake ya uendeshaji yalifika tamati Julai 2021 na mgodi huo ulifungwa rasmi Julai 2022.
Ujumbe wa Burkina Faso uliokuwa na ziara ya siku sita nchini, pamoja na vikao vya kitaalamu na Wizara ya Madini, ulitembelea mikoa na maeneo mbalimbali ya shughuli za madini ikiwemo Tabora, Kahama (Buzwagi) na Geita Gold Mine.
Ziara hizo zinalenga kuwapa wajumbe fursa ya kujifunza kwa vitendo kuhusu usimamizi wa shughuli za uchimbaji, uendeshaji wa migodi, uongezaji thamani wa madini, pamoja na mifumo ya udhibiti na usimamizi wa sekta kwa tija na uwazi.




EmoticonEmoticon