MGOMBEA UBUNGE NLD AIKUMBUSHA SERIKALI KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

February 17, 2026




Na Boniface Gideon, TANGA 


Aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Tanga katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025 kupitia chama  cha National League for Democracy ( NLD ), Ramadhani Mwikalo,ameitaka serikali kuwakumbuka Vijana kwakuwawezesha kiuchumi hususani katika sekta ya Teknolojia ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira.


Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Tanga ,mara baada ya kuwasili nchini akitokea nchini China alikogudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa kampuni ya Sinoma (Suzhou) Construction Co., Limited inayojihusha na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Viwanda, Vituo vya Gas, na Usfirishaji.


Mwikalo alisema,endapo Taifa litaweka mikakati imara ya kuwawezesha Vijana nchini hususani katika sekta ya Teknolojia ni rahisi zaidi kuondoa changamo za ukosefu wa ajira nchini,


"Sote tunaona kwenye mataifa ya wenzetu wamewekeza sana kwenye Teknolojia,hii imewasaidia sana kwenye mataifa yao kuongeza kiwango cha ajira, Vijana wamekuwa wabunifu wa kutengeneza bidhaa mbalimbali kuanzia wakiwa wadogo,hii imewasaidia kuinua uchumi wa nchi zao na uchumi wa Vijana wenyewe" Aliongeza Mwikalo 


Alisema Mkutano huo wa wiki moja  uliwakutanisha viongozi, wataalamu na wadau mbalimbal Miongoni mwa ajenda kuu zilizojadiliwa ni fursa za uwekezaji katika sekta za ujenzi na uchimbaji madini, sekta ambazo zimeendelea kuwa mhimili muhimu wa maendeleo ya Taifa.


"Tumejadiliana kwa undani fursa za uwekezaji katika ujenzi na madini na namna Teknolojia inavyochukua nafasi kubwa katika sekta ya uchumi Duniani,hivyo nitumie fursa hii hii kuikumbusha Serikali,kuona umuhimu wa kuwawezesha Vijana nchini katika Teknolojia ili kuimarisha uchumi wao" Alisisitiza Mwikalo



                    MWISHO

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »