WAZIRI NDEJEMBI AKUTANA NA BALOZI WA OMAN,WAJADILI MASUALA YA MAFUTA NA GESI

February 17, 2026


Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani yaliyolenga kuimarisha na kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta ya nishati. Mazungumzo hayo yamefanyika leo, tarehe 17 Februari 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, wamejadili kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kubadilishana uzoefu wa kitaalamu, mafunzo kwa wataalamu, teknolojia ya uchimbaji pamoja na usimamizi wa miradi ya gesi na mafuta kwa lengo la kuharakisha maendeleo kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Shirika la Maendeleo ya Mafuta la Oman (PDO).


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »