MEYA TANGA ATOA WITO KWA VIJANA WANAOPATA FURSA YA AJIRA NJE YA NCHI

January 28, 2026





Na Oscar Assenga,TANGA

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Seleboss Mustapha amewataka vijana wataopata fursa ya ajira nje ya nchi katika Falme za Kiarabu kufanya kazi kwa uadilifu na kuitangaza vizuri sifa na fursa ya nchi jambo ambalo litafungua milango kwa wengine kuendelea kuaminiwa.

Seleboss aliyasema hayo  wakati akizungumza na vijana zaidi ya 200 waliojitokeza kufanyiwa usaili kwa ajli ya kwenda nchi za falme za Kiarabu kwa shughuli za udereva wa pikipiki maarufu kama Bodaboda.

Alisema kufanya kazi kwa uaminifu sambamba na kuyaishi maadili ya kitanzania katika nchi za kigeni itasaidia kuleta taswra njema ya kutangaza nchi kwa mazuri badala ya kuwa kinyume chake.

Aidha alisema watakaofanikiwa kupita kwenye mchujo wakawe mabalozi wazuri kwa kufanya kazi lea ajil ya maendeleo yao ikiwemo kutokusahau kuwekeza nyumbani ikiwemo wawwe waaminifu

Meya huyo aliwataka kuhakikisha wanazingatia sheria na tararubu na miongozo ya nchi wanazokwenda ili waweze kufanya shughuli vizuri lakini kwa kujenga imani kwa wengine kuweza kuvutika na vijana kutoka nchni.

Awali akizungumza Ofisa Kazi Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Mahusiano Peter Ugata alisema kwamba Serikali imekuwa ikiendelea kuratibu fursa za ajira nje ya nchi kwa kuhakiisha wanawasimamia vijana wao kupata ajira zao.

Alisema kuwa hiyo ni dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa vijana na hivyo ni muhimu vijana kuchangamkia fursa hizo zinapojitokeza.

Alisema miongoni mwa majukumu yao ni kuhakikisha wanapata vijana wenye sifa na vigezo ambao wataweza kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu za nchi husika.

Naye kwa upande wake mmoja wa vijana wanaoshiriki kwenye usaili huo ,Juma Haki waliishukuru Serikali kwa fursa hiyo kuweza kufika hadi ngazi ya mikoa na hivyo kuweza kushiriki nao.

Hata hivyo alisema kwamba wanaishukuru Serikali kwa fursa hiyo ambayo itasaidia kumaliza changamoto za ajira lakini itawapa mwamko wa kujipanga kwa ajili ya kuwa na sifa za kufanya kazi nje ya nchi .


Mwisho.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »