Muonekano wa bwawa la kuhifadhi maji taka katika mgodi wa Barrick North Mara (Picha kutoka Maktaba)
Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa Maji kutoka Wizara ya Maji Bw. Heri Chisute akifungua mkutano huo
Meneja Ufungaji Mgodi wa Barrick Buzwagi Mhandisi Zonnastraal Mumbi akifuatilia mada
Baadhi ya washiriki katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
Baadhi ya washiriki katika picha ya pamoja wakati wa mkutano huo
**
Kampuni ya Barrick nchini imeeleza dhamira yake ya kuendelea kutekeleza na kufuata kanuni za sheria za Afya na utunzaji wa Mazingira na ndio maana imewekeza kujenga mabwawa ya takasumu (TSF) katika migodi yake kwa viwango vya kimataifa ili kuhakikisha wafanyakazi wake na jamii nzima zinazozunguka maeneo ya migodi haziathiriki kwa namna yoyote na taka zitokanazo na mchakato wa uzalishaji dhahabu.
Hayo yamebainishwa na Meneja Ufungaji Mgodi wa Barrick Buzwagi Mhandisi Zonnastraal Mumbi, katika mkutano wa utunzaji mabwawa unaoendelea jijini Mwanza na kuhusisha wadau mbalimbali ambapo alisisitiza kuwa licha ya kampuni kuwekeza kujenga mabwawa ya kuhifadhi taka sumu kwa viwango vya kimataifa katika migodi ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa, bado imekuwa ikifanya ufuatiaji mkubwa wa mabwawa hayo kuendana na sera ya kampuni ya afya, usalama na utunzaji wa mazingira.
“Kampuni imekuwa na mipango madhubuti kuhakikisha mabwawa ya taka sumu hayaleti madhara kwa wafanyakazi pamoja na jamii inayozunguka migodi sambamba na kuhakikisha sheria na miongozo ya nchi kuhusiana na utunzaji wa mabwawa haya inafuatwa wakati wote na kushirikiana na taasisi za Serikali zinazosimamia Mazingira na Afya na Usalama Mahali pa Kazi. Hii ni pamoja na uchambuzi wa visima vya maji ya kunywa na vyanzo vya maji ya juu ya ardhi vinavyozunguka mgodi”, alisema Mumbi.
Aliipongeza Serikali kwa kuandaa mafunzo na semina za mara kwa mara kuhusiana na usimamizi wa mabwawa ya maji na mabwawa ya takasumu kwa kuwa yanawezesha wadau kukutana na kubadilishana mawazo ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na kukosekana na umakini katika kuyatunza vilevile kufana mipango thabiti ya utunzaji wa mazingira.
Akifungua semina hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa Maji kutoka Wizara ya Maji Bw. Heri Chisute, alisema Serikali inaendelea kuhakikisha ujenzi wa mabwawa ya takasumu unafanyika kwa viwango na kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji, pamoja na usalama.




EmoticonEmoticon