WAKILI JUDITH KAPINGA AKABIDHIWA RASMI ILANI YA UCHAGUZI

September 22, 2025

 


đź—“️ *21 Septemba,2025* 


📍 *Mbinga,Ruvuma* 🇹🇿.


📌 *Ndugu.Kapinga ampongeza Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2020/2025* 


📌 *Ndugu.Kapinga awaombea Kura,Dkt.Samia,Wabunge wa ccm na Madiwani* 


🟢🟢Mgombea Ubunge kupitia CCM Jimbo la Mbinga Vijijini, *Ndugu.Judith Kapinga* tarehe *21 Septemba,2025* Wilayani Mbinga amekabidhiwa rasmi na Mgombea Urais wa Tanzania, *Ndugu.Dkt.Samia Suluhu Hassan* Ilani ya Uchaguzi ya *2025/2030* ikiwa ni ishara ya kwenda kutekeleza mambo mbalimbali ya Maendeleo kwa Wananchi wa Jimbo la Mbinga Vijijini katika kipindi cha Miaka Mitano 2025-2030✍️.


🟢🟢 *Ndugu.Kapinga* amemshukuru na kumpongeza Mgombea Urais wa Tanzania, *Ndugu.Dkt.Samia Suluhu Hassan* kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa Watanzania hususani Jimbo la Mbinga Vijijini kwa kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Uboreshaji wa Miundombinu ya Barabara,Afya,Elimu na Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia,yote haya yamefanikiwa kupitia usimamizi mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020-2025.

 *Ndugu.Kapinga* ameyasema hayo Mbinga Mjini wakati wa Ziara ya Kampeni za CCM aliyoifanya Mgombea Urais, *Ndugu.Dkt.Samia Suluhu Hassan* alipozungumza na Maelfu ya Wananchi wa Wilaya ya Mbinga✍️.


🟢🟢 *Ndugu.Judith Kapinga* amewaombea Kura, *Ndugu.Dkt.Samia Suluhu Hassan* Mgombea Urais wa Tanzania,Wabunge pamoja na Madiwani✍️


     *Imetolewa na Ofisi ya Mgombea Ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini,leo tarehe 22.09.2025*

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »