🗓️ *10 Septemba,2025.*
📍 *Mbinga-Ruvuma* 🇹🇿🌍
📌 *Kapinga asisitiza Wananchi kuwachagua Viongozi wanaotokana na ccm.Rais,Wabunge na Madiwani*
📌 *Kapinga asisitiza Miradi mingi ya Maendeleo iliyotekelezwa na Rais,Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan*
📌 *Kapinga awaahidi Wananchi kufatilia Miradi mbalimbali ya Maendeleo*
🔴🔴Mgombea Ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini kupitia CCM, *Ndugu.Judith Kapinga* leo tarehe 10 Septemba,2025 katika Kata ya Ruanda-Jimbo la Mbinga Vijijini,Wilayani Mbinga amewaomba Wananchi kukichagua Chama Cha Mapinduzi kwa kura za Kishindo katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika 29 Oktoba,2025✍️
🔴🔴Ndugu, *Judith Kapinga* ameyasema hayo alipofanya Ziara ya Kampeni ya kuomba Kura kwa Wananchi Katika Vijiji vya Ukombozi,Ntunduwaro,Ruanda na Paradiso vilivyopo Kata ya Ruanda-Jimbo la Mbinga Vijijini.Kapinga akizungumza na Wananchi amesema CCM chini ya Rais, *Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan* imetekeleza miradi mingi ya Maendeleo hivyo amewaomba Wananchi kuendelea kuiamini ccm na kuchagua Viongozi wanaotokana na ccm yani,Rais,Wabunge na Madiwani✍️
🔴🔴Sambamba na hilo, *Ndugu.Judith Kapinga* amewaeleza Wananchi kuwa anatambua Changamoto mbalimbali zinazowakabili kama vile Miundombinu ya Barabara,Changamoto za Maji,Changamoto za Umeme na Changamoto za Afya ikiwemo upungufu wa Vifaa Tiba,uhaba wa Wataalamu na uchache wa Zahanati.Hivyo amewaahidi Wananchi kufatilia kwa ukaribu changamoto hizo atakapochaguliwa kuwa Mbunge✍️.
*Imetolewa na Ofisi ya Mgombea Ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini,leo tarehe 10.09.2025*
EmoticonEmoticon