DKT.SAMIA SULUHU HASSANI KARIBU TANGA,UMETENDA MAZURI MENGI,OCTOBA 29 TUNARUNDIKA KURA ZOTE KWAKO

September 23, 2025




Na Mwandishi Wetu, Tanga


Mgombea Urais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea na kampeni za kuomba ridhaa ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mikoa mbalimbali hapa nchini.


Dkt. Samia Suluhu Hassan anainadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2025-2030, anawaeleza wananchi mambo mazuri ya maendeleo yaliyomo katika Ilani hiyo ambayo ni chachu ya kusukuma mbele maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla. 


Septemba 28, 2025, ni zamu ya mkoa wa Tanga ambapo Dkt. Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya siku tatu na katika ziara hiyo, atafanya mikutano mbalimbali ya siasa katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Tanga kuomba ridhaa yeye pamoja na wabunge na madiwani watokanao na CCM.


Binafsi, niungane na viongozi wa Chama mkoa wa Tanga kumkaribisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani Tanga ni salama sana. Tanga ni nyumbani kwake. Watu wa Tanga wanampenda sana. Mapenzi yao kwake yamekuwa makubwa sana kutokana na namna ulivyoupa kipaumbele mkoa wa Tanga katika miradi mingi ya maendeleo ukigusa sekta za elimu, afya, maji, umeme, mifugo, barabara, viwanda, masoko, kilimo, madini, utalii, Bandari ya Tanga, mikopo kwa vijana, wanawake na wenye mahitaji maalum, kutaja kwa uchache. Kazi nyingi na kubwa zimefanyika Tanga, mwenye macho anajionea mwenyewe.


Nakumbuka Februari 23, 2025, Dkt. Samia alifanya ziara ya kikazi mkoani Tanga kwa muda wa siku tisa,  ambapo alitembelea wilaya zote za mkoa wa Tanga, kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambapo kwa wakati huo, serikali ilikuwa imetoa shilingi Trilioni 3.1 kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.


Katika Ziara hiyo, Dkt. Samia alisema "Ziara yangu hii imelenga kuangalia Shilingi 3.1 Trilioni zimefanya kazi gani. Nitakwenda kila wilaya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na natarajia kuzungumza na wananchi". Miezi saba imepita tangu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan afanye ziara Tanga, na sasa anarudi tena kama Mgombea Urais ambaye anaomba ridhaa ya wananchi ili aendeleze pale alipoishia katika kugusa maisha ya wananchi kimaendeleo.


Septemba 22, 2025, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MCC) Ustadhi Rajabu Abdurahman alizungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari katika Ofisi ya CCM mkoa ambapo alitoa rai kwa wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kumpokea Mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameutendea haki mkoa wa Tanga kimaendeleo.


"Niwaombe wananchi na wana CCM wote kila mmoja tunawakaribisha kumlaki na kumpokea Mgombea wa Urais kupitia CCM, hatua mgombea mwengine zaidi ya Dkt. Samia, tujitokeze kwa wingi na baada ya kumalizia mikutano Tanga Mjini atapitia Muheza, Korogwe na ratiba katika maeneo hayo zitazolewa kwa nyakati tofauti," alisema.


Wakazi wa mkoa wa Tanga wana kila sababu ya kujitokeza kwa wingi kumpokea Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani amefanya mengi mazuri ya maendeleo. Katika mikutano atakayoifanya, wananchi watapata fursa ya kusikiliza sera nzuri za CCM ambazo zitakuwa chachu ya kuharakisha maendeleo. Naamini kutokana na mengi mazuri yaliyofanyika mkoani Tanga, wananchi watapiga kura nyingi, watamrundikia kura za kutosha katika masanduku ya kura kumchagua yeye kuwa Rais lakini pia na wabunge na madiwani watokanao na CCM.

Mwisho

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »