>Kutua mkoani Tanga Septemba 28 kwa ajili ya Kampeni kwa muda wa siku tatu.
>Wananchi watakiwa kujitokeza kwa wingi kumlaki.
Na Oscar Assenga, TANGA
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Alhaj Rajab Abdurhaman amesema kwamba mgombea Urais wa Chama hicho Dkt. Samia Suluhu ni kiongozi aliyejipambanua kuwaletea watanzania maendeleo kutokana na kasi ya utendaji wake.
Rajabu ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (MCC) aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo kuhusu ujio wa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Samia Suluhu mkoani humo kwa ajili ya kampeni kwa muda wa siku tatu.
Alisema kwamba Dkt Samia atapokelewa Septemba 28 Jioni mwaka huu eneo la Mkata wilayani Handeni atawasalimia wananchi wa mkoa wa Tanga kupitia eneo hilo baadae atakwenda Tanga mjini kwa ajili ya mapumziko na siku inayofuatia ataanzia wilaya ya Pangani kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara na Tanga mjini
Alisema kwamba anayokuja kuwahutubia kupitia ilani ya uchaguzi 2025/2030 baada ya kuunda Serikali maendeleo yatakayokuja kwa ajili ya wananchi wote hiyo niwaombe wana CCM wote popote walipoo kila mmoja wanawakaribisha kujitokeza kumlaki mgombea huyo.
“Niwaombe wananchi na wana CCM wote kila mmoja tunawakaribisha kumlaki na kumpokea Mgombea wa Urais kupitia CCM hatuna mgombea mwengine zaidi ya Dkt Samia tujitokeza kwa wingi na baada ya kumalizia Mkutano Tanga mjini atapita Muheza, Korogwe na ratiba katika maeneo hayo zitatolewa kwa nyakati tofauti”Alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha alisema kwamba wana Tanga wanajiona watu wenye bahati kupata ugeni huo mkubwa kwa mara ya pili kwa mwaka huu mmoja amekuja kwa ziara ya kikazi miezi michache iliyopita mwaka huu na alikpokuja Tanga mambo mengi ya kimaendeleo ya Tanga yamefunguka na mambo yalikwenda vizuri na sasa anakuja kama Mgombea Urais.
Rajabu alisema kwamba wananchi kwenye mkoa wa Tanga wanategemea maendeleo zaidi kwa sababu kuna utofauti kati ya Mgombea wa CCM na wengine kutokana na kwamba wao walihaidi na wameshafanya kupitia ilani ya uchaguzi na aliyekuwa mtekelezaji ni Rais Dkt Samia Suluhu.
Alisema kwamba kutokana na mambo makubwa ya kimaendeleo yaliyokwisha kufanyika imani yao ni kwamba wananchi watakiunga mkono chama chao kwa sababu wana imani kwamba wakihaidi wanatekeleza kwa vitendo.
Hata hivyo alisema kwamba ni wana matumaini makubwa watu watampa kura nyingi Rais Dkt Samia Suluhu kwa sababu namna alivyojipambanua katika suala la kulinda amani ya nchi kwa kutumia busara na hekima na miradi mikubwa ya maendeleo.
Alisema kwamba Dkt Samia alipokuja katika ziara ya kikazi kabla ya kuja kuna miradi ilikuwa inasuasua lakini baada ya kuja ipi miradi imefunguka mfano barabara ya Tanga-Sadani -Bagamoto kasi ilivyoongezeka na Barabara ya Soni –Bumbuli mpaka Dindira na Korogwe kupitia kwa Meta wameona barabara hiyo wataalamu wanakwenda kuanza muda msio mrefu.
Aliongeza kwamba hiyo yote ni baada ya ujio wake hivyo wanaamini anapokuja anakwenda kuwaidi yale yaliyopo kwenye ilani mpya ya uchaguzi na miradi iliyobaki itakwenda kutiliwa mkazo itamalizika na miradi mipya iweze kuanzishwa .
Mwisho

EmoticonEmoticon