Na Oscar Assenga, MKINGA
SERIKALI ya Tanzania na Kenya wamezindua rasmi maunganisho ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCCL) na kuunganisha Mkongo wa Mawasiliano Baharini inayopitia Mombasa kupitia Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (ICTA).
Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Habari,Mawasiliano na Uchumi wa Kenya Mhandisi William Gitau pamoja na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Tanzania Jerry Silaa ambapo walisema kwamba hatua ya uzinduzi huo ni nzuri kutokana na kwamba italeta faida kwa Mataifa yote mawili.
Alisema kwamba wanapongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kazi nzuri na kubwa ambayo imewezesha mpango huo na kueleza hatua ya kuunganisha mkongo wa mawasiliano kati ya Tanzania na Kenya ulikamilika tokea mwezi Januari mwaka huu na kuanzia Aprili Mosi mwaka huu mawasiliano yalianza kupita baina yay Tanzania na Kenya .
Aidha alisema kwamba Serikali imeweza kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji kukuza matumizi ya tehama na kidigitali sambamba na kufungua fursa kwa nchi za Jumuiya za Afrika Mashariki na Jumuya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC kutumia miundombinu iliyopo ya mkongo wa Taifa ya Mawasiliano na wao wanaendelea kutekeleza maelekezo yake aliyoyatoa Desemba 10 2024.
“Kazi ya kujenga Miundombinu ya nchi moja ni kazi moja lakini ukibaki nayo haina faida yoyote ni kama nyumba umejenga na kuweka wayaringi lakini haujaweka umeme kutoka Tanesco kazi tunayoifanya ni kuhakikishaa miundombinu ya Kenya na Tanzania na iliyopo chini ya bahari kama ulivyosema Kenya imeunganika na Sauth Sudani inaunganika pamoja”Alisema
Waziri Silaa alisema kwamba Mkurugenzi wa TTCL alisema vizuri tayari leo wameunganisha na Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi,Malawi ,Mozambiq na Zambia na sasa wanaanza mradi mkubwa wa kupitisha kebo chini ya ziwa Tanganyika kuunganisha Tanzania na Kongo DRC maunganiko yaliyofanywa leo kwa upande wa Tanzania yameunganishwa na nchi sita hivyo ni kazi kubwa ya kupongezwa sana
Aliongeza kwamba Rais Dkt Samia Suluhu Julai 29 mwaka 2024 alizindua mkakati wa uchumi wa kidigitali Tanzania na moja kati ya nguzo sita ni nguzo ya miundombinu na kinachofanyika ni moja ya maelekezo yake yaliyopo kwenye mkakati huo ya kuhakikisha miundombinu ya mawasiliano inaimarika.
“Kuunganisha miundombinu hii zipo faida nyingi faida ya kwanza pale Dar Tanzania tunaunganika na mikongo iliyopo chini ya habari ambayo ni matatu wenzetu wa Kenya Mombasa wameunganika na mikongo ya bahari nane na kwa miunganiko ya leo Tanzania wanapata fursa ya kuweza kuunganika na mikongo nane iliyopo Mombasa ambalo ni jambo kubwa sana”Alisema .
Akiziungumzia Faida ya kuunganika kwa mikondo ni uhakika wa mtandao na kama watakumbuka mwaka jana walipata tatizo la kukatika mkongo wa chini ya bahari uliounganika Dar na hivyo kupelekea kukosekana kwa mtandao (Internet) kwa nchi hivyo kuchati kunakuwa hakuna na ukikosa mtandao benki miamala inakuwa hakuna ,uongozaji wa ndege,kukata tiketi na biashara na utalii ni jambo kubwa kwenye dunia ya leo.
Hata hivyo alisema kuunganika na njia hiyo kwenda Kenya maana yake tatizo lolote linaloweza kujitokeza kwenye mkongo unaoingia Dar maana yake watanzania wataendelea watapata mawasiliano kupitia mikongo inayoingia inayoputia Mombasa vilevile kupata hitilafu kwa mkongo unaoingia Mombasa basa wakenya watapata mawasiliano kwa mikongo inayopita Dar.
Alisema faida nyengine ni ni gharama nafuu na hivyo kuchochea biashara na vijana kupitia bunifu,utalii kuongezekana na milango ya biashara inafunguka na nimataumia yake watanzania na wakenya watatumia muunganiko huo kwa faida ya biashara kwa nchi mbili.
Awali akizungumza Waziri wa Mawasiliano wa Kenya William Kabogo alisema uzinduzi wa mkongo huo ni hatua muhimu kwa mataifa yote mawili hasa katika kuimarisha huduma za mawasiliano ya uhakika na kupunguza changamoto za kukatikatika kwa mtandao
Alisema jambo la msingi ni ushirikiano kwa nchi zote mbili kwa kuhakikisha wanaitunza miundombinu hiyo ya kimkakati ili kuepuka uharibifu unaoweza kusababisha kukatika kwa umeme na mtandao.
“Lakini jambo hilo lisiishie kwenye maunganisho ya leo leo bali wafike maeneo mengi ya Namanga,Holili na mengine tuongeze wigo kwa nchi mbili na yatusaidie kufanya diplomasia ya kiuchumi,kidigitali na ninaimani jambo hili linawezekana “Alisema
Mwisho.
EmoticonEmoticon