TANESCO YAANZA KAMPENI YA KUTOA ELIMU YA USALAMA KWENYE MATUMIZI YA UMEME MIKOA YA KANDA YA ZIWA

March 29, 2025


📌Kampeni inalenga kuelimisha watoto kuzingatia usalama kwanza watumiapo umeme. 


📌Itasaidia Kupunguza athari na ajali zitokanazo na majanga ya umeme kwenye Mikoa hiyo.

Shirika la Umeme Tanzania  (TANESCO) Machi 27 limeanza kampeni maalumu ya kuelimisha juu ya kuzingatia usalama kwanza kwenye matumizi ya Umeme kwa Makundi ya watoto katika shule mbalimbali za msingi zilizopo kwenye mikoa ya Mara, Kagera, Mwanza, Geita na Simiyu.

Kampeni hiyo inayoitwa " Zingatia Usalama Kwanza Utumiapo Umeme" inalenga kuwafikia wanafunzi wa shule za msingi na kuwapa elimu inayowawezesha kugundua vihatarishi vinavyoweza kusababisha ajali zinazotokana na majanga ya umeme na kuepuka  athari zitokanazo na majanga hayo.

Akizungumza katika moja ya Shule zilizotembelewa Kaimu Meneja Masoko kutoka TANESCO Bwana Sylvester Matiku amesema elimu hiyo ni muhimu kuwalinda watoto na majanga ya umeme kutokana na kuwa kati ya makundi yanayopata athari zaidi na ajali za umeme.

''Shirika limeona lianze kampeni hii hasa kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na hivi karibuni kuwa na matukio ya ajali zitokanazo na umeme zinazoathiri zaidi watoto na hivyo tukaona tuje kuwaelimisha ili kusaidia kupunguza na kuondoa madhara ya ajali zitokanazo na umeme''.

Wanafunzi hao wamepatiwa elimu kuhusu Matumizi Sahihi ya Umeme ili kuokoa gharama pamoja na kuitambulisha namba mpya ya ya huduma kwa wateja bila malipo ya Mchongo 180.

Katika kampeni hiyo Wanafunzi katika  shule mbalimbali wamepata fursa ya kuhoji maswali kuhusu umeme na athari za umeme na jinsi ya kumsaidia muathirika wa ajali za umeme.

Wanafunzi hao wameahidi kufikisha elimu waliyoipata kuhusu Umeme na Usalama katika Kampeni ya hiyo kwa familia zao, ndugu, jamaa na marafiki na wameomba elimu hiyo pia ifikishwe kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum.

Kampeni hii muhimu inaendelea kwenye mikoa yote Kwenye Kanda ya Ziwa.



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng