Na Jane Edward, Arusha
Naibu Waziri wa Fedha Hamad Chande amewataka wahitimu kuwa waaminifu sehemu za kazi kwani hiyo ni moja ya nguzo ya kupata maendeleo yanayotakiwa kwenye jamii.
Akizungumza na wahitimu wa chuo cha Uhasibu Arusha katika mahafali ya 26 ya chuo hicho amesema amefurahishwa na wahitimu hao kwani wengi wao ni watumishi katika serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Chande amesema kuwa anaupongeza Uongozi wa IAA kwa kuanzisha ushirikiano na Shule ya Polisi Moshi kutoa kozi za masuala mbalimbali yakiwemo Usalama na amani pamoja na Ulinzi wa taarifa, na kusisitiza kuwa kozi hizo zinatolewa kimkakati ili kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya ulinzi na usalama.
Prof. Eliamani Sedoyeka ni Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA), amesema pamoja na kujitanua ndani ya nchi, dhamira ya IAA pia ni kujipambanua Kimataifa.
Aidha amesema kuwa chuo kimeshafanya ziara za kimkakati nchini mbalimbali ikiwemo Comoro, Sudan Kusini, China na Uingereza ili kufanya mazungumzo na baadhi ya Vyuo Vikuu vya Elimu ya juu kuona namna wanavyoweza kushirikiana katika utoaji wa mafunzo kwa viwango vya kimataifa.
" IAA itaendelea kuanzisha mitaala inayokidhi mahitaji ya Soko la Ajira Kitaifa na Kimataifa na kubabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia"alisema.
EmoticonEmoticon