ZANZIBAR YAJIDHATITI KUJENGA MIUNDOMBINU YA MICHEZO

November 03, 2024

 


Na. Mwandishi Wetu Zanzibar, Zanzibar.

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar  Hemed Suleiman Abdulla amesema kuwa, Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya ya michezo Visiwani Zanzibar na kuboresha vivutio vya Utalii ili kuweza kuitangaza Zanzibar kimataifa na kuwavutia wanamichezo maarufu Duniani.

Ameyasema hayo kwa niaba ya Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi wakati wa kukabidhi zawadi kwa washiriki wa Tigo/Zantel Zanzibar International Marathon yaliyofanyika katika viwanja vya Forodhani jijini  Zanzibar.

Amesema kuwa serikali ipo katika hatua ya kuimarisha miundombinu  ya michezo kwa kuanza na ujenzi wa Uwanja mkubwa utatumika katika mashindano ya Afcon 2027 pamoja na  kuvifanyia  ukarabati mkubwa viwanja vya New Amani Complex na Uwanja wa Gombani Stadium Pemba.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais ametumia fursa kwa Kuwataka  wanamichezo na wananchi kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa hiari kwa kudai risiti wanaponunua bidhaa na kwa upande wa wafanyabiashara kutoa risiti wanapofanya mauzo jambo litakalosaidia kuziba myanya ya upotevu wa mapato ya Serikali na kuweza kupiga hatua kimaendeleo.

Mapema Mdhamini wa Zanzibar International Marathon Afisa Mkuu wa Biashara Tigo Zantel Isack Nchunda amesema kuwa antaendelea kudhamini mashindano mengine ili kuiunga mkono serikali ya awamu ya Nane  ( 8 ) sambamba na kuviendeleza vipaji vilivyopo nchini kupitia michezo mbali mbali.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »