RC MTAKA AISHUKURU TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA UTAPIAMLO NA UDUMAVU KWA WATOTO MKOANI NJOMBE

February 28, 2024

Na Issa Michuzi

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, ameishukuru Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) kwa kukubali kushiriki katika kukabiliana na changamoto za utapiamlo na udumavu wa watoto mkoani humo.

Mkuu huyo wa Mkoa alitoa kauli hiyo baada ya mkutano wake na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya JMKF, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Makao Makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es salaam uliofanyika Jumanne jioni.

Katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa Mtaka ambaye aliambatana na Katibu Tawala wake Bi. Judica Omary na Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Juma Mfanga, alisema msaada wa JMKF utasaidia pakubwa katika kupambana na changamoto hiyo.

“Hivi sasa tuko katika kampeni ya kuelimisha umma kuhusu tatizo hilo na kutoa majibu ya nini kifanyike kuepukana na janga hilo….

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ametuelekeza tufanye juu chini kutafuta suluhu ya kudumu ya changamoto hii na ahadi ya Taasisi ya JMKF kusaidia jitihada za serikali kupambana na tatizo hilo ni jambo la kushukuriwa sana.

“Kwa kuchangisha rasilimali, utaalamu, na kujenga ushirikiano wa kimkakati, kuna matumaini ya kupatikana maendeleo makubwa yanayoweza kuboresha hali ya lishe na ustawi wa watoto wa mkoa wetu", alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Wengine walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na Patrick Codija, Mkuu wa Lishe pamoja na Bi. Ophilia Karumuna, Afisa, wote kutoka Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF).

Wengine ni Vanessa Anyotti, Afisa Mtendaji Mkuu na Dkt. Catherine Sanga kutoka Taasisi ya JMKF, Germana Leyna wa Kituo cha Chakula na Lishe Tanzania, na Dkt. Nyambura Moremi, Kiongozi wa Idara ya Utafiti wa Maabara ya Afya ya Umma ya George Mwita, Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Lishe ya Kimataifa (Nutrition International), pia alishiriki pamoja na Bernard Makene kutoka Taasisi hiyo yenye makao yake makuu nchini Canada.

Awali, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mfanga alimweleza Dkt. Kikwete kwamba licha ya uwezo mkubwa sana wa kuzalisha mazao ya chakula, bado zaidi ya asilimia 50 ya watoto wa Mkoa wa Njombe wanakabiliwa na tatizo la utapiamlo, na hivyo kuwasababishia udumavu, unyafuzi na ukondefu.

Katika maelezo yake, RMO aliongeza kuwa chanzo kikuu cha tatizo hilo ni kwamba wazazi wengi hawana muda wala maarifa ya kuandaa lishe bora kwa ajili ya watoto wao.

"Hali hii inapelekea wazazi kutegemea zaidi unga wa mahindi kuandaa chakula cha kila siku licha ya kuwepo kwa matunda na mboga za lishe mbalimbali."

“Kwa hiyo, unakuta watoto wanakoseshwa virutubisho muhimu hali inayosababisha udumavu, kinga dhaifu, na kuongezeka kwa hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali", alifafamua Dkt. Mfanga.

Aidha, alibainisha changamoto hiyo hujidhihirisha katika kiwango cha juu cha udumavu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, ambapo takribani nusu yao wameathirika.

"Hali hii haidumazi tu ukuaji wa kimwili wa mtoto bali pia inaathiri ukuaji wa kiakili, kinga, na ustawi wa jumla," alisema Dkt. Mfanga.

Kwa upande wake Rais Mstaafu Dkt. Kikwete alieleza kuwa ameguswa na takwimu za hivi karibuni zinazoonesha ukubwa wa tatizo hilo, hususan katika Mkoa wa Njombe.

Aidha, alieleza pia kufurahishwa na juhudi za makusudi zinazofanywa na uongozi wa Mkoa wa Njombe katika kukabiliana na changamoto hiyo.

Alitumia pia fursa hiyo kueleza kuwa miongoni mwa malengo ya Taaisi yake ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) ni kulinda na kukuza afya ya uzazi na Watoto.

Hiivyo, alibainisha, mkutano huo umetoa fursa nzuri kwa upande wa Taasisi yake kupata taarifa muhimu zitakazosaidia kupanga mikakati ya kuweza kushirikiana na Serikali na wadau wengine katika kukabiliana na tatizo hilo la utapiamlo nchini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF), Rais Mstaafu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka kabla ya kuanza kwa mkutano wao katika makao makuu ya JMKF Masaki jijini Dar Jumanne jioni. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi Judica Omary.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF), Rais Mstaafu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, katika mkutano na  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka na ujumbe wake katika makao makuu ya JMKF Masaki jijini Dar Jumanne jioni. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi Judica Omary.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF), Rais Mstaafu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipokea Ripoti ya hali ya Lishe Pamoja na Kalenda toka kwa  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka baada ya mkutano wao katika makao makuu ya JMKF Masaki jijini Dar Jumanne jioni. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi Judica Omary.



Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF), Rais Mstaafu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipokea Ripoti ya hali ya Lishe Pamoja na Kalenda toka kwa  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka baada ya mkutano wao katika makao makuu ya JMKF Masaki jijini Dar Jumanne jioni. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi Judica Omary.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi Ripoti ya Lishe Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) , Bi. Vanessa Anyoti, baada ya mkutano  katika makao makuu ya JMKF Masaki jijini Dar Jumanne jioni.

Picha na JMKF

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF), Rais Mstaafu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, katika

Picha ya Pamoja na na  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka na ujumbe wake katika makao makuu ya JMKF Masaki jijini Dar Jumanne jioni.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »