MHE. KAPINGA : TANOIL IMARISHENI UTENDAJI KAZI KULETA MATOKEO CHANYA

January 05, 2024


Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni Tanzu ya Mafuta ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakati wa ziara yake ya kikazi katika kampuni hiyo Tarehe 05 Januari 2024 Jijini Dar es salaam.



Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akitoa maelekezo kwa Bodi na Manejimenti ya Kampuni Tanzu ya Mafuta (TANOIL) wakati wa ziara yake ya kikazi Tarehe 05 Januari, 2024 Jijini Dar Es Salaam.




Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni Tanzu ya Mafuta (TANOIL), Patrick Mongela akieleza utendaji kazi wa Kampuni hiyo kwa Naibu Waziri Nishati Mhe. Judith Kapinga wakati wa ziara yake ya kikazi Tarehe 05 Januari, 2024 Jijini Dar Es Salaam.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Kampuni Tanzu ya Mafuta(TANOIL), wakati wa ziara yake ya kikazi Tarehe 05 Januari, 2024 Jijini Dar Es Salaam.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Manejimenti ya Kampuni Tanzu ya Mafuta(TANOIL), wakati wa ziara yake ya kikazi, Tarehe 05 Januari, 2024 Jijini Dar Es Salaam.



Dar es Salaam,

Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni Tanzu ya Mafuta (TANOIL) ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Menejimenti ya Kampuni hiyo wameaswa kuhakikisha kuwa wanaimarisha na kuleta matokeo chanya kiutendaji yanayofanywa na kampuni hiyo kwa watanzania na Taifa kwa jumla.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kampuni hiyo, Tarehe 5 Januari, 2024, Jijini Dar es Salaam.

Ameileza Bodi na Menejimenti kuwa wahakikishe TANOIL inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Malengo, Dhima na Azma ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo nchini.

Vilevile ameelekeza kuwa Viongozi hao watumie Mbinu zao, Taaluma na Uwezo Wao wote kuhakikisha kuwa Kampuni hiyo inatengeneza faida zaidi badala ya hasara kwa taifa na pia waepuke kuzalisha madeni.

Aidha ameelekeza TANOIL kushirikiana na TPDC, Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Maji na Mafuta (EWURA) katika kutekeleza majukumu yao kwa kuwa yanashabihiana ili kuleta matokeo chanya ya kampuni hiyo katika kujiendesha.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »