WAMSHUKURU RAIS DKT SAMIA SULUHU KWA KUKUZA UHUSIANO KATI YA CHINA NA TANZANIA

December 04, 2023





Na Oscar Assenga, MUHEZA

TAASISI ya Tanzania China Friendship wameshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kufanya kazi kubwa kukuza uhusiano huo mkubwa uliopo kati ya China na Tanzania

Hayo yamesemwa leo na Mwakilishi wa Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam wanaofanya kazi na Ubalozi wa China nchini Husna Abdurhaman Sharif wakati wa halfa ya kukabidhi msaada wa vitanda 24 katika Hospitali ya wilaya ya Muheza vyenye thamani ya Milioni 16.1.

Msaada huo ni kuunga mkono juhudi za Mbunge wa Jimbo la Muheza Hamisi Mwinjuma “Mwana FA ambaye amekuwa akipambana usiku na mchana kuhakikisha anawapa maendeleo wakazi wa Jimbo hilo.

Alisema kwa sababu ndani ya mwaka mmoja tayari amekutana na Rais wa China mara mbili na amekuwa kipenzi cha wachina wengi barani Afrika hivyo wanampongeza Rais samia kwa kazi kubwa ya kuwapa maendeleo nchini.

“Hii ni hatua kubwa sana hivyo tuna kila sababu ya kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha anawapa maendeleo watanzania “Alisema

Msaada huo ulitolewa kufuatia ombi la Mbunge huyo wa Muheza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Michezo Utamaduni na Sanaa hivyo nao wakaona wamuunge mkono hasa katika kusaidia sekta ya afya kwenye Hospitali ya wilaya kwa wakina mama na watoto.

“Kwani wakina mama duniana kote wana changamoto na tumeona tutoe msaada wa vitanda kwa wakina mama wajifungue salama na vitenda kazi vyengine na hii ni kiufuatia ombi la Mbunge wenu na hasa na urafiki wa kihistoria kati ya Tanzania na China nchi hizi ni marafiki wakubwa”Alisema Husna

Alisema taasisi yao ya Tanzania China Friendship wamekuwa wakitoa misaada nchi nzima katika Sekta ya Afya,Elimu na Teknolojia kuenzi urafiki huo mkubwa

Alisema kwamba wakina mama kwa ujumla wao kama taasisi wapo tayari kushirikiana na majimbo mbalimbali ambayo yatapeleka maombi ya ufadhili hata kwa fursa ya kwenda kusoma nje ya nchi na safari ya maendeleo ni ndefu lakini watafika na leo wanatoa vitanda vya aina tatu.

Awali Mbunge wa Jimbo la Muheza Hamisi Mwinjuma alimaarufu Mwana FA-aliishukuru Taasisi hiyo kwa kuamua kuwasaidia wananchi ikiwemo kusikia kusikia kilio chao ambacho walikiwasilisha kwao.

Alisema kwamba siku zote wanasema wanazungumzia hospitali hiyo na wana juhudi za kuwa na Hospitali ya wilaya ya Muheza huku akieleza ina historia kubwa akiwamo Rais Samia.

Alisema kwa sasa wana juhudi za kuhakikisha wanakuwa na Hospitali ya wilaya ya Muheza wakati wanakwenda kwenye uchaguzi 2025 wanataka wawe na kitu tofauti na kile ambazo walikikuta mwaka 2020.

Alisema na namna bora ya kuwa kiongozi wakati wanakwenda kwenye uchaguzi wawe wamefanya mabadiliko makubwa katika maendeleo tofauti na walivyoomba mara ya kwanza.

Aidha alisema wao kama viongozi kazi yao ni kutafuta suluhu hya matatizo ya wananchi ikiwemo yatakayojitokeza mapya wakati wanapokwenda kuomba tena ridhaa ya wananchi kwa mara nyengine.

“Matatizo yaje lakini yawe …Hospitali ni fursa ya kuonyesha kuna kitu tunafanya ndio maana tunahaingaika na ndugu zetu hawa wa Tanzania China Friendship wamesikia kilio chetu na kutusaidia”Alisema Mbunge Mwana FA.

Katika hatua nyengine Mbunge hiyo alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuwapatia fedha kiasi cha Bilioni 3.7 kwa ajili ya Hospitali hiyo na bado wanaendelea kumuomba na wanajua kwa moyo wake wataendelea kupata zaidi.

“Ukija miaka miwili ijayo tutakuwa na Hospitali ya wilaya ya Samia Suluhu iliyokamilika,tunakushukuru na tunaendelea kukuomba mtusaidie kutushika mkono na DMO ataweza kuorodhesha mahitaji ili mtakapoweza mtusaidie”Alisema

Naye kwa upande wake,Katibu wa CCM wilaya ya Muheza alisema wanamshukuru Mbunge wao kwa sababu bado anahangaikia kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.

“Nikupongeze Mbunge wetu ambaye amekuwa ukifanya kazi kubwa kuhakikisha wana Muheza wanapata maendeleo makubwa sana na sisi Muheza tunaupendeleo wa kuletewa maendeleo kwa sababu ya juhudi zako mbunge hivyo nikuombe uweke nguvu kubwa sana kuhakikisha majengo yaliyopo kwenye eneo hilo la Hospitali yanamalizika”Alisema

Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »