Na Oscar Assenga, TANGA
JUMUIYA ya Wazazi ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga imepongeza Spika wa Bunge Dkt Tulia
Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) huku
wakihaidi kuendelea kumuunga mkono na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu katika
majukumu yake hayo.
Pongezi hizo
zilitolewa leo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Hamza Bwanga
wakati akizungumza na mtandao huo ambapo alisema kwamba wanaamini kwamba
kuchaguliwa kwake kumekuja wakati muafaka kutokana na utendaji wake mahiri
katika kuongoza Bunge la Tanzania.
Alisema kuchaguliwa
kwake ni kutokana na jitihada zake katika utendaji wake ambao umejengwa na
uchapakazi, uzoefu, uaminifu na uadilifu ambao umekuwa ni chachu kubwa kufikia
mafanikio hayo.
“Sisi kama Wazazi
wilaya ya Tanga tunakupongeza sana Spika wa Bunge kuwa kuchaguliwa kwake kuwa
Rais wa umoja huo na tunahaidi kumuunga mkono na nafasi hii imekuja wakati
muafaka kabisa kwa kuwa yeye ni spika na mchakapazi,mwerevu msikivu “Alisema
Hata hivyo alisema
kwamba wao wataendelea kumuunga mkono na kumuombe kwa mwenyezi mungu ili kutenda
vema majukumu yake kwa waledi mkubwa .
EmoticonEmoticon