Katibu wa Mbunge jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Thomas Daffa amewataka vijana wa wilaya hiyo kutumia vyema fursa ya kilimo aliyoitoa Mbunge wa jimbo hilo Mhe Salim Alaudin Hasham ili wainuke kiuchumi.
Daffa amesema ni wakati wa vijana sasa kutumia kilimo kama njia ya kubadilisha maisha yao kiuchumi kwani kwasasa kilimo kimekuwa ni Njia ya mafanikio katika maeneo mengi duniani.
Pia Daffa amesema kwa Fursa ambayo Mbunge wa jimbo hilo ameitoa kwa vijana kuwa atawalimia mashamba yao bure kwa kutumia trekta zake binafsi ni vyema sasa kwa vijana kuacha kukaa vijiweni na kupiga soga badala yake waingie shambani kwani Taifa linawategemea sana.
Siku za hivi karibuni Mbunge Salim Hasham alisema atatoa trekta zake kuwalimia vijana bure mashamba yao hivyo kila kijana anayetaka kulimishiwa basi afike kwenye ofisi yake ili aweze kupatiwa msaada huo kwa lengo la kuhakikisha vijana wanajiajiri na kupunguza tatizo la ajira wilayani humo.
Aidha Daffa amewasisitiza vijana kuacha kutumika kuvuruga amani ya nchi ambayo imetunzwa na waasisi wetu na badala yake ni muda wa kufanya vitu vyenye tija kwa jamii na Taifa letu kwa ujumla.
Daffa pia ameongoza harambee ya ujenzi wa ofisi ya Chama cha Mapinduzi kata ya kichangani na kuweza kukusanya kiasi cha Mil 3,222,000/= ambayo itaanzisha ujenzi huo ili mpaka kufikia mwezi disemba basi kata hio iweze kupata ofisi ya chama.
Jimbo la Ulanga Lina jumla ya kata 21 na vijiji 159 hivyo chama cha Mapinduzi kinafanya hivyo kujiimarisha kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 na ule uchaguzi mkuu 2025.
EmoticonEmoticon