FCC :YABAINI ASILIMIA 3.4 YA MAKONTENA HAYAJAFATA SHERIA YA ALAMA YA BIDHAA BANDARINI

August 02, 2023




Na Hamida Ramadhan , Dodoma

MKURUNGEZI Mkuu wa Tume ya Ushindani FCC William Erio amesema wameendelea kufanya Kaguzi ili kubaini wanaoingiza bidhaa nchini zilizo kiuka Sheria ya alama za bidhaa.

Pia FCC imefanya kaguzi ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu (ICDs) ambapo 3.4% ya jumla ya makasha (containers) yaliyokaguliwa yenye thamani ya kiasi cha Shilingi Bilioni 20.8 yalikutwa na bidhaa zilizokiuka Sheria ya Alama za Bidhaa .

Mkurungezi huyo ameyasema hayo leo Jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utendajiwa majukumu ya FCC ambapo ameeleza Kaguzi za kushtukiza (Dawn Raids) zilifanyika  bidhaa zenye thamani ya Shilingi Billioni 4.7 zilizokiuka Sheria ya Alama za Bidhaa zilikamatwa na hatua stahiki zilichukuliwa. 

Amesema Kaguzi hizo zilifanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Ruvuma, Songwe, Kilimanjaro, Pwani, Mwanza, Arusha, Katavi na Mbeya.FCC imefanya uharibifu wa bidhaa bandia zilizokamatwa katika Mikoa ya Mbeya, Iringa na Ruvuma. 

Amebainisha bidhaa zilizoharibiwa ni pamoja na wino wa printa katoni 432 na kilo 1,302 za vifungashio.Kaguzi hizi zinapunguza madhara ya bidhaa bandia ambazo pamoja na mambo mengine, zinaweza kutokuwa salama kwa walaji, zinaikosesha serikali mapato, na zinaweza kuathiri biashara na uwekezaji halali.

"Walaji wanatakiwa kufahamu kuwa, watengenezaji wa bidhaa bandia huwa wanazalisha bidhaa hizi kwenye brands ambazo zinauzika kwa urahisi na zenye kukubalika zaidi sokoni (reputable brands)," Amesema Mkurungezi huyo 

Na kuongeza"Hivyo  ni vizuri walaji wajifunze mbinu za kuzitambua bidhaa bandia kwa kufanya milinganisho ya bei (kati ya bandia na isiyo bandia) pamoja na kufuata maelekezo ya alama za bidhaa zinazotolewa na kampuni husika inayomiliki nembo ya bidhaa halali," amesema. 

Katika kipindi Julai, 2022 hadi Juni, 2023; FCC imefanikiwa kutekeleza na imeidhinisha maombi 56 ya miungano ya kampuni kutoka katika sekta mbalimbali kama vile kilimo, uzalishaji, madini, mawasiliano, mafuta na Gesi. 

Amesema Maombi 51 yalipitishwa bila masharti na maombi matano (5) yalipitishwa kwa masharti. Kwa mujibu wa Sheria, maombi ya miungano yanatakiwa kushughulikia ndani ya siku 90, lakini yamekuwa yakishughulikiwa kwa wastani wa siku 75.

Amesema FCC imetoa msamaha katika mkataba mmoja (1) uliokuwa ukififisha ushindani “exemption to agreement” kati ya Precision Air Services Plc na Kenya Airways Plc kwa lengo la kuendeleza Sekta Ndogo ya Usafiri wa Anga Nchini.

Ameeleza FCC imefanya uchunguzi wa mashauri 20 yanayohusu miungano ya kampuni ambayo haikuidhinishwa na FCC (unnotified mergers).

"Kati ya mashauri haya 4 yameshafungwa na yaliyobaki yako katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa. FCC imechunguza Mashauri nane (8) yanayohusu uwezekano wa kuwa na matumizi mabaya ya nguvu ya soko (abuse of market power) ambapo moja limefungwa na mengine yako katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa," amesema.

MAFANIKIO YA TUME YA USHINDANI KWA UJUMLA  

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita (mwaka 2020 - 2023), FCC iliridhia kununuliwa kwa kampuni 14 zenye jumla ya thamani ya bei ya mauziano inayofikia Shilingi Bilioni 49.4 katika sekta ya kilimo kwa lengo la kuruhusu kampuni hizo kuongeza wigo zaidi sokoni, kuongeza mitaji na kupunguza uwezekano wa kampuni hizo kuondoka sokoni.  

Kampuni hizi ni pamoja na Mtanga Foods Limited (yenye biashara zake Iringa), kampuni ya uzalishaji wa Parachichi ya Rungwe Avocado Company Limited, kampuni ya uchenjuaji mpunga (mchele) ya MW Rice Millers Limited na Mring’a Estates Limited. 


Mwisho

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »