MADAKTARI BINGWA KUTOKA NCHINI UJERUMANI WAWASILI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA BOMBO

July 14, 2023
Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Rashid Suleiman katikati akiwa na madaktari kutoka nchini Ujerumani waliowasili kwa ajili ya  kutoa huduma za kibingwa za kurekebisha Maumbile (Plastic Surgery).
Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Rashid Suleiman katikati akiwa na madaktari kutoka nchini Ujerumani waliowasili kwa ajili ya  kutoa huduma za kibingwa za kurekebisha Maumbile (Plastic Surgery).

Sehemu ya wananchi wakisubiri huduma 



Na Mwandishi Wetu, Tanga

MADAKTARI Bingwa kutoka nchini Ujerumani wamewasili katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga-Bombo kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa za kurekebisha Maumbile (Plastic Surgery).

Akizungumza leo mara baada ya kuwasili katika Hospitali hiyo,Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Rashid Suleiman alisema kwamba madaktari hao wamekuwa wakishirikiana nao na kwa sasa ni mwaka wa 13 tokea wameanza ushirikianao huo

Alisema kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo Dkt Naima Yusuf aliwashukuru Hospitali kwa matayarisho yaliyofanyika ikiwemo sapoti kwa uongozi kuanzia ngazi ya wizara kupitia Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wanashukuru .

Hata hivyo alisema kwamba wote waliofanya usajili wataonwa na kufanyiwa uchunguzi wa awali kwa kushirikiana na madaktari waliopo hapa hospitali hiyo.

Awali akizungumza Mratibu wa Kambi ya Upasuaji wa Kurekebisha maumbile (Plastic Surgery) katika Hospitali hiyo Dkt Wallace Karata alisema kwamba baada ya kuwasili hospitalini hapo wameanza kufanya uchunguzi wa awali na baadae kupangiwa ratiba tayari kwa ajili ya upasuaji .

Dkt Karata alisema kwamba wanawashukuru wananchi kwa kuitikia wito na zaidi ya wagonjwa 250 wamejiandikisha na wataonwa leo na siku ya kesho kwa ajili ya kupangiwa siku ya zoezi la upasuaji

Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »