BODI ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala
wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wametembelea Hifadhi ya Mazingira
Asilia Amani iliyopo Muheza mkoani Tanga lengo likiwa ni kukagua
uboreshaji wa miundombinu na huduma za kiutalii ambapo imelidhishwa na
hatua iliyofikiwa pamoja na uwekezaji uliofanyika.
Wakati wa
ziara hiyo wajumbe wa bodi walilidhishwa na uwekezaji mkubwa uliofanyika
wa miundombinu na mazingira ya hifadhi uliofanywa na fedha za Uviko 19
lakini pia bajeti binafsi kuboresha maeneo yaliosalia.
Akizungumza
mara baada ya kukagua miradi na vivutio vya utalii vya hifadhi hiyo,
mjumbe wa Bodi Wakili Msomi Piensia Christopher Kiure aliupongeza
uongozi wa TFS kwa uwekezaji mkubwa waliofanya kwenye hifadhi hiyo na
kuutaka kuongeza ubunifu katika kuitangaza hifadhi hiyo.
Amesema
uwekezaji mkubwa umeshafanyika na sasa ni wakati wa kuhakikisha
kunakuwepo na mikakati thabiti ya kujitangaza huku akiwataka maafisa
utalii kuwa wabunifu na kusimamia utekelezaji wa malengo kwa hali
yoyote.
“Uwekezaji uliofanyika hapa ni mkubwa sana, hifadhi ina
vivutio vingi na miundombinu imeimarika ongezeni nguvu ya kuitangaza,
maafisa utalii, wengi wenu ni vijana onyesheni mnatosha, kuweni
wabunifu, toeni mawazo na muwe tayari kuyasimamia, na sio lazima lazima
uwe na fedha kuanza hili,” anasema Wakili Msomi Kiure.
Aidha,
Wakili Msomi Kiure aliutaka uongozi kuingia mikataba (MOU) na nchi
zinazofanya vizuri kwenye utalii ikolojia ili kuwe na utaratibu wa
kubadirishana wataalamu lengo likiwa ni kubadirishana ujuzi.
Kwa
upande wake, Mjumbe wa Bodi CPA. Bahati Lucas Masila aliupongeza uongozi
wa TFS kwa kuhifadhi na kuhakikisha miundombinu ya utalii hifadhini
hapo inaboreshwa na kuahidi kutumia sehemu ya likizo yake kudhuru na
familia yake kupumzika kwa kile alichosema kuvutiwa na hali ya utulivu.
Someni
Mteleka ni Mkuu wa Kitengo cha Utalii TFS anasema katika kuhakikisha
uwekezaji uliofanyika unakuwa wenye tija, pamoja na mambo mengine tayari
wameandaa video za lugha nne tofauti (Kichina, Kijerumani, Kingereza na
Kiswahili) lengo likiwa ni kuwafikia watalii wengi zaidi huku
wakifungua njia ya Amani kwenda Hifadhi ya Nilo iliyopo Lushoto.
Naye
Naibu Kamishana Msaidizi TFS na Mhasibu Mkuu Peter Mwakosya anasema
katika mwaka huu wa fedha, Wakala imetenga fedha kwa ajili ya kuboresha
zaidi hifadhi zake ili kuwavutia watalii wengi zaidi na hivyo kuchangia
katika kufikia idadi ya watalii 5,000,000 hadi ifikapo 2025 iliyowekwa
na Serikali huku mapato yakiongezeka. Tulizo Kilaga anaripoti.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon