Na John Walter-Manyara
Kampeni
ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa
Manyara imeanza kwa kasi kwa kutoa elimu ya Kujitambua kwa Wanafunzi wa
Shule za Msingi na Sekondari, kujua Ukatili na kuripoti wanapofanyiwa au
kuona mtu akifanyiwa Ukatili.
Katibu wa SMAUJATA mkoa wa Manyara
ambaye pia ni Mkuu wa Dawati la jinsia Mkoa, Willnes Kimario amewataka
wanafunzi kuwafichua wazazi ,walezi na wote wanaofanya ukatili dhidi
yao.
Pia amewataka wakawe mabalozi kwa wazazi wao kuwaambia juu ya madhara ya Ukeketaji na Ukatili mwingine kama walivyofundishwa.
Afisa
Maendeleo ya jamii Wilaya ya Babati Agatha Patrice amewaasa wanafunzi
wasiwe rahisi kukubali lifti wanazopewa barabarani au Chipsi kwani ndo
chanzo Cha kufanyiwa Ukatili na kukatisha masomo yao.
Amesema Mtoto wa kike na wa Kiume wote wana haki sawa na wanapaswa kulindwa.
Amesema
jamii ikishirikiana vyema na wadau wa kupinga Ukatili pamoja na jeshi
la polisi itaongeza nguvu katika kupunguza vitendo hivyo na wahusika
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya
Babati Philipo Sulle, amesema upo Ukatili ambao unafanywa pia na
Wanafunzi wenyewe kwa wenyewe ukiwemo Ukatili wa kihisia kwa kusemana
vibaya na kuwaonya wenye tabia hiyo waache mara Moja.
Ametoa wito
kwa wazazi kuongeza usimamizi wa karibu kwa watoto wao ili kuwaepusha
na matukio hayo na walimu kuendelea kusisitiza maadili mema yanayofuata
tamaduni za Kitanzania.
Mkuu wa shule ya Sekondari Dabil Alfred
Sulle, amesema licha ya shule hiyo kutokuwa Mhanga wa Ukatili lakini
shule nyingi Za Kata ya Dabil zinatajwa kuwa na Wanafunzi waliokumbana
na adha ya Ukatili wa aina mbalimbali.
Mkuu Dawati la Jinsia na
Watoto wilaya ya Babati mkaguzi msaidizi wa polisi Daudi Danyesi
amewataka wanafunzi na wananchi kwa Ujumla kuendelea kutoa taarifa kwa
jeshi hilo ili wahusika wakamatwe na washughulikiwe kwa mujibu wa
sheria.
Wanafunzi wameshukuru kwa elimu hiyo na kuahidi kuwa
mabalozi wazuri Kwa jamii.Mkoa wa Manyara kitakwimu katika Ukatili wa
kikinsia unatajwa kushika nafasi ya pili huku kwa Ukeketaji ukishika
nafasi ya kwanza Kitaifa.
Ukanda wa Tarafa ya Bashnet ndo unaotajwa kuongoza kwa vitendo vya Ukatili huku kesi zikimalizwa kinyumbani.
SMAUJATA
Manyara wametoa elimu hiyo katika Shule tano za wilaya ya Babati
Dabil Sekondari, shule ya Msingi Mandi, Shule ya Msingi Barmot, Shule ya
Msingi Sabilo na Shule ya Msingi Lomhong.
Kiongozi mwingine aliyekuwa kwenye jopo la watoa elimu ni Katibu msaidizi SMAUJATA Mkoa wa Manyara Rest George Chuhila
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon