Na John Mapepele
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa pongezi
kwa Timu ya Tanzania ya Wanawake ya Kriketi kwa kutwaa Ubingwa leo
Juni 18, 2022 kwenye mashindano ya Kwibuka Cup nchini Rwanda,
yaliyoshirikisha nchi nane ( Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana ,
Nigeria, Brazil na Ujerumani) bila kufungwa na timu yoyote.
Aidha, amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa anaoutoa katika michezo.
Amesema
hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha michezo kwa kuweka
mikakati kabambe chini ya uongozi wa Samia imeleta matokeo chanya
kwenye sekta za michezo na sanaa hapa nchini.
Amesema
taarifa ya hali ya uchumi wa nchi iliyosomwa bungeni hivi karibuni
imeonesha kuwa sanaa na burudani zimechangia kwa asilimia 19.4 katika
kipindi cha mwaka 2021 na kuziacha kwa mbali sekta mbalimbali.
Amesema
dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuifanya michezo kuwa uchumi badala
mazoe ya kuifanya michezo kama kitu cha burudani pekee.
Aidha,
amesema Serikali tayari inazigharimia timu zote za taifa zinazojiandaa
kwa ajili ya mashindano ya kimataifa kwa kuziweka kambini kuanzia mwanzo
wa mwaka huu.
Hivi
karibuni Mhe. Mchengerwa amekaririwa vyombo vya habari akisisitiza kuwa
michezo na sanaa ni uchumi hivyo wanamichezo na wasanii wanapaswa
kutambua kuwa vipaji walivyonavyo ni mtaji wa maisha yao.
Ujumbe
wa Klabu ya Southampton uliokutana na Mhe. Waziri Mchengerwa na kufanya
mazungumzo ya kuinua michezo ulioongozwa na Mkuu wa Idara ya Biashara
ya klabu hiyo David Thomas pia ulimpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan
kwa kazi kubwa anayoifanya kwenye michezo na kumzawadia jezi ambayo
ilipokelewa kwa niaba yake na Mhe. Mchengerwa.
EmoticonEmoticon