Wadau
mbalimbali wa kupigania maendeleo ya mtoto wa kike nchini wamejitokeza
kuchangia takribani shilingi bilioni moja kwenye taasisi ya
Mwanamke Initiative Foundation (MIF) iliyopo Zanzibar inayojishughulisha
na kumkwamua mtoto wa kike katika elimu ili kutimiza ndoto zake.
Wadau
hao wametoa michango hiyo katika halfa maalum ya chakula cha usiku
iliyoandaliwa na taasisi ya (MIF) usiku wa kuamkia leo Juni 19, 2022
Zanzibar kutokana na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na mfuko huo
katika suala zima la kuwasaidia Watoto wa kike kufikia malengo yao
hivyo kuendesha maisha yao.
Mwenyekiti
na Mwanzilishi wa Mfuko huo, Mhe. Wanu Hafidh Ameir ambaye pia ni
Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na mtetezi wa haki za vijana
na wanawake amewashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza ambapo amewaomba
kuendelea kuchangia ili kuwasaidia Watoto wa kike waweze kutimiza
ndoto zao.
“Naomba
kuchukua fursa hii kushukuru sana isiwe mwanzo wala mwisho naomba iwe
mwanzo na tuendelee kuchangia mfuko wetu wa Mwanamke Initiative ili
kuona kwamba mtoto wa kike anasimama na anaweza kushindana katika
ulimwengu” amefafanua, Mhe Wanu.
Wakitoa
maoni yao kwa nyakati tofauti tofauti kuhusu kuanzishwa kwa mfuko huo,
wamepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na MIF kwa kuwasaidia watoto wa
kike Zanzibar huku wakitoa rai kwa wadau wengi zaidi kushiriki kwenye
jitihada hizo za kuwakomboa Watoto wa kike kwa kuchangia kwa hali na
mali katika mfuko huo ili lengo liweze kutimia.
“Tumefarijika
sana na kazi kubwa na nzuri zinazofanywa na mfuko huu, tunaomba na
wadau wengine waendelee kujitokeza kuchangia kwa kuwa ukimsaidia mtoto
wa kike aweze kujikwamua umesaidia taifa”aliongeza Tuli Mwambapa ambaye
ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB nchini.
Benki ya CRDB imechangia shilingi milioni mia tatu ambapo wadau wengine pia waliweza kuchangia kwenye hafla hiyo.
Katika
hafla hiyo mbali na wageni mbalimbali waliohudhuria pia Waziri wa
Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Omary Mchengerwa ambaye ni
mume wa Wanu alishiriki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan. leo, Juni 19, 2022 anatarajiwa kuuzindua rasmi mfuko huo.
EmoticonEmoticon