Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa akiongea na
waandishi wa Habari baada ya mkutano na watumishi wa Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji na wahandisi wa Umwagiliaji wa Mikoa, uliofanyika Jijini
Dodoma mapema leo.
Mkurugenzi
Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa na Baadhi ya
watumishi wa Tume hiyo pamoja na wahandisi wa Umwagiliaji wa mikoa
Baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakifuatilia kikao kilichofanyika jijini Dodoma mapema leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Raymond Mndolwa amesema, kutakuwa na kilimo cha umwagiliaji cha uhakika kutokana na uwekezaji mkubwa wakihistoria unaofanywa na serikali ya awamu ya sita katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji.
Bw,Mndolwa ameyasema hayo mbele ya Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dodoma mara baada ya kufungua kikao kazi kilichowahusisha watumishi wote wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kuongeza kuwa, kutokana na majukumu makubwa iliyopewa na serikali Tume ya Taifa ya Umwagiliaji “niliona ni muhimu sana tukutane watumishi wote ili tujipange,tuweze kutekeleza majukumu hayo”.
“Tume tuna juku la kuwasaidia wakulima waweze kulima kutokana na kilimo wanacholima ili waweze kupata maji katika mazao wanayolima hili ni sehemu ya majukumu yetu, kutokana na hali yakuwa na upungufu wa mvua serikali imeweka msisitizo mkubwa katika kilimo cha umwagiliaji kwa matarajio yajayo”.
Tunataka Wananchi na Wakulima waliokata tamaa ya kulima warudi shambani, kwasababu tume ya Taifa ya Umwagiliaji imewezeshwa na inakuja kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo cha Umwagiliaji.
Akizungumzia suala la Bajeti kubwa iliyoelekezwa na Serikali ya awamu ya sita katika Sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji, Mkurugenzi Mndolwa ameongeza kusema kuwa, Tume imeelekeza nguvu katika miradi iliyokwisha buniwa na miradi hiyo ndiyo ya kipaumbele, baada ya miradi hiyo ya mwaka huu hatua itakayofuata ni kujenga miradi mingine ya umwagiliaji nchini katika maana ya mikoa yote itakayotekeleza kilimo cha umwagiliaji na aina gani ya miradi ifanyike katika kuhakikisha kila Mkoa na Wilaya inapata miradi ya Kilimo cha Umwagiliaji.
Alisema wana panga upya kuhakikisha kwamba mwaka wa fedha unaofuata yaani 23/24 watakuwa na mkakati ambao utaenea nchinzima.
Mwaka wa fedha huu 22/23 watarekebisha Skimu thelathini (30) za kilimo cha umwagiliaji lakini Wahandisi wa umwagiliaji wa mikoa watafanya mapitio ya miradi iliyokwisha kwa lengo la maboresho kulinga na na bajeti yetu.
“Nina ahidi kwamba maboresho yatakuwa makubwa ili kila mwananchi anayetaka kulima aweze kulima.”Alisisita Kikao cha leo ni majumuisho ya siku yapili ya kikao kilichohusisha watumishiwa Tume Makao makuu na Wahandisi wa Umwagiliaji wa mikoa kilichojadili, Mpango mkakati wa miaka mitano wa utekelezaji wa shughuli zaTume.
EmoticonEmoticon