KAMPUNI YA KILIMANJARO SAR LTD YAINGIA MAKUBALIANO NA HOSPTALI YA ST JOSEPH YA KUTOA HUDUMA KWA WATALII WALIPATA MATATIZO MLIMA KILIMANJARO

March 14, 2018
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kilimanjao SAR ,Ivan Braun akitia saini makubaliano ya Mashirikiano na Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi kuhusu uanzishwaji wa Kliniki ya utoaji matibabu kwa Wagonjwa wanaopata matatizo wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro na Meru,kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya St Joseph ,Sister ,Urbanie Lyimo huku zoezi hilo likishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba (aliyesimama kulia) ,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya (katikati) na kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Kilimanjaro SAR,Amour Abdallah.
Zoezi hilo la utiaji saini pia lilifanywa na Mganga Mfawidi wa Hospitali ya St Joseph ,Sister Urbanie Lyimo kwa niaba ya Hospitali.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kilimanjao SAR ,Ivan Braun na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya St Joseph ,Sister ,Urbanie Lyimo wakibadilishana karatasi zenye makubaliano ya kushirikiana katika utoaji wa matibabu kwa Wagonjwa waliopata matatizo kutokana na hali ya muinuko katika Mlima mara baada ya kutia saini .
Mkuu wa wilaya ya Moshi akizungumza wakati wa Hafla fupi ya utiaji saini wa makubaliano hayo .
Baadhi ya Wauguzi na Madaktari katika Hosptali ya St Joseph wakifuatilia zoezi la utiaji saini wa makubaliano hayo .
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya akizungumza wakati wa hafla hiyo .
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kilimanjao SAR ,Ivan Braun akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hosptali ya St Joseph mjini Moshi.
Mganga Mfawidi wa Hospitali ya St Joseph ,Sister Urbanie Lyimo akitoa wasifu wa Hosptali ya St Joseph wakai wa hafla fupi ya utiaji saini wa makubaliano ya mashirikiano na Kampuni ya Kilimanjaro SAR.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Kilimanjaro SAR,Amour Abdalah akizungumza katika Hafla hiyo.
Mgeni rasmi katika Hafla hiyo,Kippi Warioba na wageni wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Wauguzi katika Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi.
Mgeni rasmi katika Hafla hiyo,Kippi Warioba na wageni wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya Kilimanjaro SAR mara baada ya kukamilika kwa zoezi la utiaji saini .

NA Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini .

SEKTA ya Utalii nchini imepata suluhu ya Changamoto ya muda mrefu ya utoaji wa msaada wa kitabibu, utafutaji na uokoaji wa wageni wanaopata matatizo wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro na Meru .
Changamoto hiyo inafika kikomo rasmi baada ya kampuni ya Kilimanjaro SAR kuzindua Kliniki ya kwanza Afrika ya magonjwa yatokanayo na muinuko wa juu pamoja na utumiaji wa Helkopta kwa ajili ya uokoaji katika Hifadhi za Mlima Kilimanjarona Mlima Meru.
Mbali na uzinduzi huo Kilimanjaro SAR imeingia makubaliano na Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi ,kuanza kutoa huduma za kitabibu kwa wagonjwa watakao pata matatizo wakati wa kupanda Milima hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa makubaliano kati ya Kampuni ya Kilimanjaro SAR na Hospitali ya St Joseph ,Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba aliyekuwa mgeni rasmi amesema hii ni fursa mpya kwa sekta ya Utalii kuutangaza vyema Mlima Kilimanjaro.
Huduma hii ya kwanza kutolewa barani Afrika inaiweka Tanzania katika nafasi ya pili katika Ramani ya Dunia, kuwa  na kliniki ya kipekee katika utoaji wa huduma kwa wapanda Mlima na kwamba kwa kiasi kikubwa itasaidia katika kuongeza idadi ya Watalii. 
Hata hivyo kuanza kwa huduma hiyo muhimu kwa sekta ya Utalii nchini ,bado ipo changamoto ya matumizi ya uwanja mdogo wa ndege wa Moshi hali inayowalazimu kutumia uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA).
Ulbanie Lyimo ni mganga Mfawidhi wa Hospitali ya St Joseph akaeleza faida itakayopatikana kutokana na kuingia makubaliano na kampuni hiyo ya Uokoaji ya Kilimanjaro SAR kuongeza maarifa katika utoaji wa matibabu kutoka kwa madaktari wa kigeni watakao hudumia wagonjwa wa Mlimani.
Kuanza kwa kliniki hii ni msaada kwa maiha ya wapandaji wa Mlima Kilimanjaro na Meru ikizingatiwa asilimia 75 ya magonjwa uwapo mlimani yanatokana na mbadiliko ya Hali ya Hewa kulingana na urefu wa Mlima.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »